Skip to main content

ZAIDI YA WAKAZI 2000 WA VIJIJI VYA BUTONDORO, JANA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA BIL. 5

Zaidi ya wakazi 2,000 wa vijiji vya Butondoro na Jana, katika Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga, wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama kupitia mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria wenye gharama ya shilingi bilioni tano.

ZAIDI YA WAKAZI 2000 WA VIJIJI VYA BUTONDORO, JANA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA BIL. 5
Studio Narration JAMBO FM

ZAIDI YA WAKAZI 2000 WA VIJIJI VYA BUTONDORO, JANA KUNUFAIKA...

0:00 --:--

Zaidi ya wakazi 2,000 wa vijiji vya Butondoro na Jana, katika Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga, wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama kupitia mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria wenye gharama ya shilingi bilioni tano.

Mradi huo unalenga kuwaondolea wakazi wa maeneo hayo adha ya kutafuta maji katika visima, huku ujenzi wake ukiendelea.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, alipotembelea Kata ya Jana kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Butondoro, Elizabeth Bundala na Laurencia Mwandu, wanaeleza changamoto wanazokutana nazo katika upatikanaji wa maji.

“Tunashukuru sana mradi huu ukikamilika yani wakazi wa Kijiji cha Butondoro tumeteseka sana kupata huduma yam aji,wakati mwingine tunachangia maji a mifugo hali inayotufanya kuugua mara kwa mara kutokana na kutumia maji yasiyo safi na salaa” Wamesema wakazi hao.

huo, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama, Mhandisi Maduhu Magili, anaeleza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo, huku Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mabula Magangila, akieleza umuhimu na manufaa yanayotarajiwa kupatikana baada ya mradi kukamilika.

“Mradi huu bado haujakamilika kutokana na ujenzi wa bomba kuu bado haujakamilikakutoka Kijiji cha Shishinuhu kuja hapa Butondolo,Mradi huu ukikamilika wakazi hawa wataondokana na adha yam aji kwani wamesumbuka muda mrefu” Amesema Magili na Mbunge wa Msalala Mh Magangila.

Kwa upande wake, Naibu wa Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, amesema kuwa mradi huo Serikali iko katika hatua utekelezaji ili wananchi waondokane na adha ya upatikanaji wa maji.

“Huu mradi unaoendelea hapa wenye thamani ya shilingi ya shilingi ya bilioni tano ambao mpaka sasa haujamilika,Mh Rais ametuelekeza kuja kutekeleza mradi na kuhakikisha tunaleta fedha kiasi cha shilingi milioni mianne na tisini zinakuja kwenye kata ya Jana” Amesema Mh Kundo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.