Skip to main content

ZAIDI YA MABOMA 1,900 VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA KUKAMILISHWA NCHINI

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu– TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya afya, Dk. Jafar Seif, amesema Serikali imeweka mpango wa kukamilisha kwa awamu maboma zaidi ya 1,900 ya zahanati na vituo vya afya yaliyojengwa na wananchi katika maeneo mbalimbali nchini, huku ikihitaji zaidi ya Shilingi bilioni 115 kutekeleza mpango huo.

Dkt. Seif ameyasema hayo leo Novemba 5, 2026, bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Nyang'hwale, Hussein Amour, aliyetaka kujua lini Serikali itasaidia kukamilisha zahanati mbili zilizojengwa kwa nguvu za wananchi katika vijiji vya Nnuigwe, Kata ya Nyamtukuza na Nyaruguguna, Kata ya Njundu, ambazo zimekaa bila kuanza kutoa huduma kwa takribani miaka minne.

Dk. Seif mesema Ofisi ya Waziri Mkuu– TAMISEMI tayari imefanya uratibu wa maboma hayo nchini na kuyaweka katika mpango wa kuyakamilisha kwa awamu ili yaanze kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha, Dkt. Seif amempongeza Mbunge huyo kwa kutumia Mfuko wa Jimbo na kushirikisha wananchi katika ujenzi wa miundombinu ya afya, akieleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha maboma hayo yanakamilika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.