Skip to main content

ZAIDI YA BIL. 25 KUKAMILISHA UJENZI BARABARA ZA LAMI KAHAMA

Na William Bundala - Kahama.

ZAIDI YA BIL. 25 KUKAMILISHA UJENZI BARABARA ZA LAMI KAHAMA

Na William Bundala - Kahama.

Wananchi wa manispaa ya Kahama mkoani Shinyaga leo wameshuhudia utiaji Saini wa mkataba wa ukamilishaji wa ujenzi wa barabara za lami na mitaro zenye urefu wa zaidi ya kilometa 20 unaotarjiwa kujengwa na kampuni ya M/S China Civil Engineering Construction Corporation

Tukio hilo limefanyika leo May 27 katika viwanja vya Phanthom vilivyopo kata ya Nyasubi Manispaa ya Kahama na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali Pamoja na wananchi wa Manispaa ya Kahama jimbo la Kahama mjini Pamoja na Halmashauri ya Ushetu na Msalala.

Kupitia hafla hiyo Serikali wilayani kahama mkoani Shinyanga, imetia saini mkataba huo wa ukamilishaji wa ujenzi wa barabara za lami na mitaro wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 25.

Mradi huo unatekelezwa kupitia mradi wa Benki ya Dunia unaojulikana kama TACTIC, na utatekelezwa na mkandarasi M/S China Civil Engineering Construction Corporation wenye kandarasi nyingine ya ujenzi wa barabara ya Kahama Kwenda Kakola.

Akizungumza katika hafla hiyo mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Mh Riziki Shemdoe amesisiza umuhimu wa usimamizi mzuri wa mradi huo ili kumaliza changamoto za miundombinu ya barabara zinazowakabili wananchi wa Kahama na kutoa wito kwa uongozi wa manispaa ya Kahama kusimamia kwa umakini ujenzi huo.

“Ofisi ya Waziri mkuu inayoshughulia tawala za mikoa na serikali za mitaa tutasimamia kwa ukaribu kabisa utekelezaji wa mradi huu,mimi sitovumilia kuona kwamba yale yaliyotokea kipindi cha nyuma yakitokea tena,waandarasi niwaambie wazi hatutohitaji nyongeza ya mud awa mkataba,” amesema Shemdoe.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Benjamin Ngayiwana, amesema suala la barabara limekuwa likimnyima usingizi kutokana na malalamiko ya wananchi huku Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani, akiomba halmashauri tatu za Wilaya ya Kahama kuajiri mameneja wa TARURA ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa sekta ya barabara.

“Mh Mgeni rasmi kila ninapopita suala ni barabara tu,kwakweli hii changamoto  imetutesa sana ikiwa masika mashimo yanajaa maji yanaingia kwenye makazi na biashara za wananchi ikiwa kiangazi vumbi kila sehemu,Ombi langu ni moja Mh Waziri Kahama tupatiwe mameneja wa TARURA kila halmashauri hii itasaidia kurahisisha usimamizi wa utendaji na ufuatiliaji wa barabara zetu” Amesema Mh Ngayiwa mbunge wa Kahama mjini na Mbunge wa Jimbo la Ushetu.

Awali akizungumza kuhusu utelekelezaji wa mradi huo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amesema kuwa ujenzi huo utakuwa na awamu mbili ambazo ni ujenzi wa barabara za kati ya mji na mifereji ya maji na awamu ya pili I ujenzi wa kituo cha mabasi Mbulu Pamoja na ujenzi wa soko la Sango na Zongomela.

“Mh waziri Ujenzi wa kwanza ni barabara za kati ya mji kwa km 12.3  pamoja na mitaro ya Mtaa wa Chelsea,Magobeko,Lyanzugu Pamoja na Shunu,Na awamu ya pili ni ujenzi wa kituo cha mabasi Mbulu Pamoja na ujenzi wa soko la Sango Pamoja na soko la eneo la viwanda Zongomela.

Kwa upande wake Naibu  mkurungenzi mkuu wa kampuni ya M/S China Civil Engineering Construction Corporation bwana Wu Zegang amesema kuwa kwasasa wana mradi mwingine wa barabara ya Kahama Kwenda Kakola a kwamba wana vifaa na watenda kazi wakutosha hivyo haitakuwa ngumu kukamilisha barabara za Kahama manispaa na kuiomba serikali ya wilaya ya Kahama kutoa pesa kwa wakati ili waanze ujenzi kwa wakati.

“Tuna vifaa na watendaji a kutosha mana tunajenga pia barabara ya Kahama Kwenda Kakola hivyo itakuwa rahisi kusimamia ujenzi huu,Kikubwa serikali itoe fedha kwa wakati ili nasi tuanze kazi kwa wakati na kukamilisha kwa wakati” Amesema Zegang.

Nao baadhi ya wananchi akiwemo Amocy Makala na Sixbeth Daudi wamesema kuwa wameteseka sana na vumbi katika barabara za Kahama na kwamba vyombo vya moto zikiwemo bajaji na pikipiki zimekwa zikiharibika mara kwa mara na kumuomba mkandarasi aliyepata tenday a ujenzi huo kuhakikisha anakamilisha ujenzi kwa wakati ili wananchi waondokane na adha zinazowakabili.

“Kwakweli tunashukuru sana,leo ndo tumeamini kuwa ujenzi unaendelea mana hizi barabara zimekuwa kero kwetu pamoja na vyombo vyetu vya usafiri,tumuombe mkandarasi huyu asiwe kama yule wa kwanza katuharibia barabara zetu akashindwa kuzimaliza” Wamesema wananchi hao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.