Skip to main content

YAFAHAMU MAZAO 'MALI' YASIYOPEWA KIPAUMBELE NA MWANADAMU

Sinq shaka utakuwa unatambua ninaposema Mazao yasiyopewa kipaumbele, licha ya kuwa na umuhimu katika maisha ya mwanadamu.

YAFAHAMU MAZAO 'MALI'  YASIYOPEWA KIPAUMBELE NA MWANADAMU
Studio Narration JAMBO FM

YAFAHAMU MAZAO 'MALI' YASIYOPEWA KIPAUMBELE NA MWANADAMU

0:00 --:--

Sinq shaka utakuwa unatambua ninaposema Mazao yasiyopewa kipaumbele, licha ya kuwa na umuhimu katika maisha ya mwanadamu.

Haya ni yale yenye afya, ambayo mara nyingi hupuuzwa au kutotumika ipasavyo, licha ya faida zake kuwa muhimu kwa uongezaji lishe na afya.

Aina hizi za mazao, huwa zipo lakini hazipati umaarufu, uwekezaji wa kutosha katika kilimo au matumizi ya lishe, ingawa yana thamani kubwa katika kuboresha afya na lishe.

Zipo sababu kadhaa zinazochangia mazao haya kutopewa kipaumbele, ikiwepo kukosa maarifa ya kutosha kuhusu faida za lishe na matumizi mazuri ya mazao hayo.

Aidha, mazao hayo pia mara nyingi hayapewi kipaumbele katika sera za kilimo au mipango ya maendeleo ya kilimo, na hivyo kuwa na uwezekano mdogo wa kupata rasilimali za kutosha kwa uzalishaji wake.

Hatq hivyo mengine huzalishwa tu kwa lengo la kuangalia soko na si kama matumizi ya lishe mfano ufuta.

Hapa nimekuandalia faida za kiafya za baadhi ya mazao muhimu yasiyopewa kipaombele kama vile njugu mawe, ulezi, ufuta, uwele, maboga, biringanya, na mchicha.

Njugu Mawe:

Zina protini, wanga, nyuzinyuzi, na madini muhimu kama vile chuma na zinki.

Protini zilizomo katika njugu mawe husaidia katika ukuaji wa tishu na misuli, wakati wanga hutoa nishati. Nyuzinyuzi husaidia katika mmeng’enyo wa chakula na kuzuia kufunga choo.

Ulezi:

Ulezi una wanga, nyuzinyuzi, madini kama kalsiamu na chuma, na pia vitamini muhimu.

Unapunguza sukari kwenye damu, kuzuia upungufu wa damu na kusaidia afya ya moyo na mifupa.

Ufuta:

Wenyewe una protini, nyuzinyuzi, mafuta yenye afya, na madini kama chuma na kalsiamu.

Mafuta mazuri ya ufuta husaidia katika afya ya moyo, wakati protini hutoa nguvu na misuli yenye nguvu.

Uwele:

Ni mzuri katika wanga, nyuzinyuzi, na vitamini muhimu kama B-complex.

Pia Uwele ni chakula bora kwa nishati na pia husaidia katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Maboga:

Yanavitamini A, C, na E, na pia madini kama kalsiamu na chuma.

Vitamini A husaidia katika afya ya macho, wakati vitamini C inaboresha kinga ya mwili na kupunguza hatari ya magonjwa.

Biringanya:

Yenyewe ina nyuzinyuzi, vitamini, na madini kama potasiamu na magnesiamu.

Nyuzinyuzi za biringanya husaidia katika utumbo mzuri, wakati vitamini na madini husaidia katika afya ya moyo na mishipa ya damu.

Mchicha:

Mchicha una protini, madini kama kalsiamu na chuma, na pia vitamini kama folate.

Protini za mchicha husaidia katika ukuaji na ukarabati wa mwili, wakati madini na vitamini husaidia katika afya ya mifupa na damu.

Ni muhimu kuingiza mazao haya katika lishe zetu ili kufaidika na faida zao za kiafya. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kufurahia afya bora na ustawi wa jumla.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.