Skip to main content

YAFAHAMU MAENEO HATARI ZAIDI DUNIANI, SABABU ZINASHANGAZA

Dunia imejaa mambo mengi mazuri na mabaya, lakini pia zipo sehemu ambazo ni nzuri kutembelea na pia za hatari nazo zinapatikana, ambazo kiuhalisia hazifai kwa binadamu kufika au kuishi huko.

YAFAHAMU MAENEO HATARI ZAIDI DUNIANI, SABABU ZINASHANGAZA
Studio Narration JAMBO FM

YAFAHAMU MAENEO HATARI ZAIDI DUNIANI, SABABU ZINASHANGAZA

0:00 --:--

Dunia imejaa mambo mengi mazuri na mabaya, lakini pia zipo sehemu ambazo ni nzuri kutembelea na pia za hatari nazo zinapatikana, ambazo kiuhalisia hazifai kwa binadamu kufika au kuishi huko.

Hapa nimekuletea baadhi ya maeneo ambayo ni hatari zaodi kwa binadamu kufika huko, nikianza na Kisiwa cha North Sentinel - Bahari ya Hindi.

Kabila la Sentinelese wanaishi huko na wanakataa kabisa kuwasiliana na watu wa nje.

Serikali ya India imekataza mtu yeyote kufika ndani ya km 5, kwani watu wa huko Wana mishale na wanaweza kukushambulia mara moja, usifike hapo ni hatari.

2. Kisiwa cha Nyoka - Ilha da Queimada Grande, Brazil.

Kinajulikana kama "Snake Island". Kuna nyoka wa aina ya Golden Lancehead zaidi ya 4000.

Sumu yao inaweza kuyeyusha nyama. Serikali ya Brazil hairuhusu watalii, wanasayansi tu na vibali maalum.

3. Unyogovu wa Danakil - Ethiopia.

Huko joto linafikia 50°C, kuna gesi za sumu zinazotoka ardhini, asidi, na mabwawa ya salfa yenye rangi ya njano.

Ni mojawapo ya sehemu zenye joto kali zaidi duniani.

Ukikosea ukavuta hewa bila barakoa unaweza kupata shida.

4. Pripyat na Chernobyl - Ukraine.

Baada ya mlipuko wa nyuklia 1986, mionzi bado ipo, na unaweza kutembelea kwa muda mfupi na watembeza watalii.

Lakini kuishi huko ni hatari kwa sababu ya saratani na magonjwa ya mionzi.

5. Oymyakon - Russia.

Hiki ni Kijiji chenye baridi zaidi duniani. Halijoto ya hapo inashuka hadi -67°C.

Wajuzi wa mambo wanadai ukiwa hapo, Mafuta ya gari yanakosa mzunguko, simu zinazimika, na ngozi inaganda ndani ya dakika chache nje.

6. Bonde la Mauti - Death Valley, USA.

Unaambiwa hapo joto linaweza kufika 56°C.

Kwanza wanasema hakuna maji eneo hilo na endapo ukipotea, dehydration inakuja haraka sana.

Kutokana na sababu hizo, inaarifiwa kuwa Watu wengi wamekufa kwa joto na upweke mara walipofika eneo hilo.

7. Mlango wa Kwenda Jehanamu - Darvaza Gas Crater, Turkmenistan.

Hapo una shimo kubwa ambalo linawaka moto tangu mwaka 1971, lakini kama mnavyowajua Bin Adam hawajawahi kufeli, wanafika hapo na kufanya utalii.

Kuna taarifa kuwa ipo Gesi ya methane ambayo inatoka chini na kusababisha mlipuko kwa juu ambao ni hatari.

Wanasema hakuna uzio kama ambavyo picha inajionesha, hivyo ukianguka ndani yake, basi hakuna kurudi tunakusahau.

8. Mabonde ya Mariana - Pasifiki.

Sehemu yenye kina kirefu zaidi baharini, ambacho kinafikia kilomita 11 chini ya maji.

Inaarifiwa kuwa hapo kuna shinikizo mara 1000 zaidi ya juu ya bahari.

Bila manowari maalum ya kukufikisha eneo hilo kiuhalisia lazima mwili utapqta shida.

Sababu kuu zinazofanya sehemu hizi ziwe hatari ni hali ya hewa, wanyama wenye sumu, mionzi, gesi za sumu au watu wasiopenda wageni.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.