Skip to main content

WMA GEITA YAJIPANGA KWA UKAGUZI, UFUATILIAJI MIZANI YA AMCOS

Na Ibrahim Rojala - Geita.

WMA GEITA YAJIPANGA KWA UKAGUZI, UFUATILIAJI MIZANI YA AMCOS

Na Ibrahim Rojala - Geita.

Wakala wa Vipimo (WMA) mkoani Geita wamejipanga kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa mizani yote inayotumiwa na wanunuzi katika Vyama vya Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS).

Meneja wa WMA mkoa wa Geita, Eva Ikula ametoa taarifa hiyo kupitia mahojiano maalum ambapo ameeleza kwamba kueleza hatua hiyo inalenga kudhibiti udanganyifu wakati wa ununuzi wa mazao na katika utekelezaji wa hatua hiyo, WMA itafanya kazi na vyama vya ushirika vyote mkoani Geita ikiwemo Chama cha Ushirika Geita (GCU), Chama Cha Ushirika Mbogwe (MBCU) na Chama Cha Ushirika Chato (CCU).

Meneja wa WMA mkoa wa Geita, Eva Ikula.

“Itapangwa ratiba maalum, mizani itahakikiwa kama inapima kwa usahihi na kuweka alama maalum ambapo hufanyika udanganyifu wa Mizani” asema Eva.

Ametaja kiashiria kikubwa cha udanganyifu kwenye mizani ni kuanza kusoma kuanzia na takwimu za juu kabla ya kuanzia chini hali inayoashiria kuwa mizani imeshasogezwa mbele akiongeza kwamba WMA itakuwa bega kwa began a wakulima katika zoezi hilo kwa kushirikiana kwa ukaribu na vyama vya ushirika.

Kwa upande wake Mrajisi Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Geita, Doreen Mwanri amesema katika kupunguza changamoto ya udanganyifu wa vipimo wamejipanga kuhakikisha wanasimamia matumizi ya mizani ya kidijitali.

Mrajisi Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Geita, Doreen Mwanri.

“Wakulima wa zao la pamba ni lazima watumie Mizani ya kidigitali na mikoa mbalimbali kama vile Shinyanga, Simiyu, Kigoma tayari wameshaanza kutumia Mizani hiyo ya kidijitali.

Akielezea faida ya mizani ya kidigijitali amesema mizani hiyo imeboreshwa na hutoa taarifa kwa muuzaji wa zao la pamba ni kilo ngapi ameuza na malipo yake ni kiasi gani hatua inayorahisisha kutuma malipo kwa benki au simu.

“Hii Mizani itasaidia kupunguza upotevu wa pesa, na kukomesha changamoto ya ucheleweshaji wa malipo kupitia kwa wanunuzi wa mazao ya tumbaku,” alisema.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.