Na Gideon Gregory - Dodoma.
Wizara ya Uchukuzi imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi trilioni 2.87 kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo yanayolenga kuimarisha sekta ya uchukuzi nchini.
Akiwasilisha bungeni leo Mei 13,2026 hotuba ya makadrio ya bajeti ya wizara hiyo mwaka wa fedha 2026/27 Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 126 zimetengwa kwa matumizi ya kawaida huku zaidi ya Shilingi trilioni 2.74 zikielekezwa katika miradi ya maendeleo.
Mhe.Mbarawa amesema fedha hizo zimekusudiwa kuendelea kuboresha miundombinu ya bandari, reli, viwanja vya ndege pamoja na huduma za usafiri wa anga na majini nchini. Katika sekta ya bandari, Serikali imeendelea kutekeleza Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam (DMGP) sambamba na maboresho ya bandari za Bagamoyo, Mtwara, Mwanza North, Mbamba Bay na Kigoma.

"Katika mwaka wa fedha 2026/27, uwekezaji huo umeendelea kupitia ununuzi wa mitambo ya kisasa ya kupakia na kupakua mizigo, ujenzi wa mageti mapya yanayounganisha bandari na Barabara ya Nelson Mandela pamoja na uwekezaji.
Aidha amesema kampuni ya DP World imeendelea kuwekeza katika vifaa vya kisasa vya kuhudumia mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza ufanisi na ushindani wa huduma za bandari.
Amesema maboresho hayo yanatarajiwa kuongeza uwezo wa kuhudumia mizigo kwa kiwango kikubwa ifikapo mwaka 2028.
Discussion
Reader comments
0 contributions