Skip to main content

WHATSAPP YABORESHA HUDUMA, WATUMIAJI WARAHISISHIWA MAWASILIANO

WhatsApp imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuongeza vipengele vipya vinavyorahisisha mawasiliano na kuongeza usalama wa watumiaji.

WHATSAPP YABORESHA HUDUMA, WATUMIAJI WARAHISISHIWA MAWASILIANO
Studio Narration JAMBO FM

WHATSAPP YABORESHA HUDUMA, WATUMIAJI WARAHISISHIWA MAWASILIA...

0:00 --:--

WhatsApp imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuongeza vipengele vipya vinavyorahisisha mawasiliano na kuongeza usalama wa watumiaji.

Maboresho hayo yanalenga kurahisisha mawasiliano ya mtumiaji kulingana na maombi na uhitaji wake kwani mtandao huo uimekuwa na kawaida ya kuchukua maoni ya nini kiboreshwe na nini kipunguzwe ili kuvutia zaidi watumiaji wake wote duniani.

1. KUPIGA SIMU KUPITIA KOMPYUTA

WhatsApp imeendelea kuboresha huduma zake kwenye kompyuta ili kurahisisha mawasiliano.

Watumiaji wanaweza kufanya shughuli mbalimbali bila kutegemea simu pekee.

Maboresho ya kupiga simu na kuzungumza kwa video yanawasaidia watu kuendelea kuwasiliana wanapokuwa kazini au wanapotumia kompyuta tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo watumiaji wangeweza kupiga simu kwa kutumia simu pekee.

2. MABORESHO YA MAKUNDI(GROUPS)

WhatsApp imeongeza njia zinazorahisisha mawasiliano kwenye makundi(groups). Watumiaji wanaweza kutumia kura kupata maoni ya wanakikundi kuhusu jambo fulani.

Maboresho haya yanaweza kusaidia familia, marafiki na wafanyakazi kufanya maamuzi kwa urahisi bila kulazimika kusoma ujumbe mwingi.

3. USALAMA WA AKAUNTI UMEBORESHWA

WhatsApp inaendelea kuboresha ulinzi wa akaunti za watumiaji ili kupunguza uwezekano wa watu wengine kuzitumia bila ruhusa.

Njia za ulinzi ni pamoja na uthibitishaji wa hatua mbili na funguo za kidijitali zinazoweza kutumia alama ya kidole au utambuzi wa uso. Watumiaji wanashauriwa pia kutowapa watu wengine namba zao za siri.

4. MAJINA YA WATUMIAJI BADALA YA NAMBA ZA SIMU(USERNAMES)

WhatsApp imekuwa ikifanyia kazi kipengele cha majina ya watumiaji, kitakachowapa watu njia nyingine ya kuwasiliana bila kulazimika kutoa namba zao za simu.

Kipengele hiki kinaweza kuwa na manufaa kwa wafanyabiashara na watu wanaokutana na wageni kupitia mtandao. Hata hivyo, upatikanaji wake hutegemea hatua ya utoaji wa huduma hiyo.

5. MATUMIZI YA AKILI MNEMBA

WhatsApp imeendelea kuingiza teknolojia ya akili mnemba katika baadhi ya huduma zake.

Teknolojia hii inaweza kusaidia kuboresha picha na kupendekeza majibu ya ujumbe, hivyo kumwezesha mtumiaji kufanya baadhi ya shughuli kwa haraka zaidi.

Hata hivyo, ni muhimu kusoma na kukagua ujumbe unaopendekezwa kabla ya kuutuma.

6. KUBORESHA MATUMIZI YA WHATSAPP

Maboresho mengine yanalenga kufanya programu iwe rahisi kutumia katika shughuli za kila siku, zikiwemo mawasiliano ya kifamilia, biashara na kazi.

Watumiaji wanashauriwa kusasisha WhatsApp kupitia duka rasmi la programu ili kupata maboresho yanayopatikana kwa simu zao.

Mabadiliko haya yanaonesha kuwa WhatsApp inaendelea kutafuta njia za kurahisisha mawasiliano na kuboresha huduma zake.

Hata hivyo, si vipengele vyote vinavyopatikana kwa kila mtumiaji kwa wakati mmoja. Ni muhimu kuangalia toleo la programu na mipangilio ya akaunti ili kujua huduma zinazopatikana.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.