Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka watoa huduma za afya kuhakikisha wananchi waliojunga na bima ya afya kwa wote wanapata huduma wanazostahili kwa mujibu wa vifurushi na masharti ya bima zao bila kunyimwa huduma au kutozwa malipo yasiyoidhinishwa.
Balozi Sirro amesema hayo leo October 21, 2026 wakati akizungumza na wanahabari kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya bima ya afya kwa wote unaotarajiwa kufanyika October 22, 2026 katika zahanati iliyopo kata Rusimbi Manispaa ya Kigoma Ujijiji.

Alisema mwanachama mwenye sifa ya kupata huduma anapaswa huduma kwa wakati pasipo kupata usumbufu.
Katika hatua nyingine Balozi Sirro alisema awamu ya kwanza ya uandikishaji wa bima ya afya kwa wote wamefanikiwa kuandikisha kwa zaidi ya asilimia 76 na matarajio kwa awamu ya pili ni kuandikisha idadi kubwa zaidi.
“Takwimu zinaonesha kuwa katika awamu ya kwanza jumla ya 11,454 zimesajiliwa kati ya kaya lengwa 15,037 huku wanufaika 33,446 sawa na asilimia 51 wakiwa wamefikiwa kati ya lengo la wanufaika 65,755” alisema Sirro
Kwa upande wake, Meneja uwekezaji kutoka Makao makuu ya nhif Boniface Nkingwa pamoja na Meneja wa NHIF mkoa wa Kigoma Gwamaka Mwakyoma wamesema changamoto walizokutana nazo kwenye awamu ya kwanza ya uandikishaji watazitumia awamu hii ya pili na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Meneja wa NHIF mkoa wa Kigoma Gwamaka Mwakyoma.
Uzinduzi wa awamu ya pili ya usajili wa bima ya afya kwa wote kwa mkoa wa Kigoma unatarajiwa kufanyika hapo kesho katika eneo la zahanati ya rusimbi Manispaa ya Kigoma ujiji ukiwa na kauli mbiu Bimika na Fahari Afya.
Discussion
Reader comments
0 contributions