Skip to main content

WENYE BIMA RUKSA KUPATA MATIBABU PANDE ZOTE ZA MUUNGANO - WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema hakuna tatizo la kimahusiano katika utoaji wa huduma za afya kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, akisisitiza kuwa wananchi wenye bima ya afya wanaruhusiwa kupata matibabu pande zote za Muungano.

Dkt. Mwigulu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea, Agnester Lambat, Bungeni Jijini Dodoma na kusema huduma za matibabu hazitolewi kwa kuzingatia mtu anatokea upande gani wa Muungano, bali kwa kufuata taratibu za mifumo ya bima ya afya.

Amesema, “kutibiwa hakuangaliwi unatokea upande gani wa Muungano. Mtanzania wa Bara akiwa na bima anatibiwa Zanzibar, na wa Zanzibar anatibiwa Tanzania Bara."

Dkt. Mwigulu ameongeza, kuwa changamoto zinazojitokeza wakati mwingine zinahusiana na watu wanaoingia nchini au kupata nyaraka kwa njia zisizo halali, jambo ambalo linaendelea kushughulikiwa na mamlaka husika ikiwemo taasisi za uhamiaji.

Aidha, amewataka Watanzania kutolifanya suala hilo kuwa chanzo cha mgawanyiko, akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya pande mbili za Muungano unaendelea kuimarika na kwamba kero nyingi za Muungano tayari zimepatiwa ufumbuzi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.