Skip to main content

WCF UWAFIKIE WAFANYAKAZI MIGODINI - DC KOMBA

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, ameutaka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kuongeza wigo wa huduma zake kwa kuwafikia wafanyakazi wengi zaidi katika sekta ya madini, hususan migodi midogo na ya kati, pamoja na sekta ya uvuvi zinazokabiliwa na vihatarishi mbalimbali vya kiusalama mahali pa kazi.

WCF UWAFIKIE WAFANYAKAZI MIGODINI - DC KOMBA

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, ameutaka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kuongeza wigo wa huduma zake kwa kuwafikia wafanyakazi wengi zaidi katika sekta ya madini, hususan migodi midogo na ya kati, pamoja na sekta ya uvuvi zinazokabiliwa na vihatarishi mbalimbali vya kiusalama mahali pa kazi.

Komba amesema sekta hizo zina idadi kubwa ya watu wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi, hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha wanapata uelewa kuhusu haki zao na namna ya kupata huduma za fidia wanapopata ajali au kuathirika kiafya kutokana na kazi zao.

“Wapo watu wengi wanapata changamoto kwenye maeneo ya machimbo,na mwisho wa siku wanahangaika namna ya kuishi baada ya kupata changamoto hizo”amebainisha DC Komba

Amesema wapo wachimbaji wengi katika maeneo ya machimbo ambao hukabiliwa na changamoto za maisha baada ya kupata ajali au kuathirika kiafya wakiwa kazini. Ameitaka WCF kuangalia namna ya kuwafikia wafanyakazi hao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo, ili kuhakikisha wananufaika na ulinzi unaotolewa na mfuko huo.

 

Mkuu huyo wa wilaya ametoa rai hiyo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa maafisa rasilimali watu na maafisa usalama mahali pa kazi, yenye lengo la kuwajengea uelewa kuhusu utendaji wa WCF, taratibu za utoaji wa taarifa za ajali na namna wafanyakazi wanavyoweza kupata fidia stahiki wanapopata madhara yanayotokana na kazi.

Kwa upande wa baadhi ya washiriki hao akiwemo Levina Ladslausi kutoka Riha Company Limited meshukuruku kupata nafas iya kushiriki mafunzo hayo na kueleza kwamba baada ya mafunzo kukamilika watahakikisha wafanyakazi wao wanasajiliwa WCF wakati Benard Semeni kutoka Kampuni ya Yunde akieleza kwamba wamekuwa wakiendelea kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa salama kwa kila mfanyakazi katika kipindi chote cha utekelezaji w wa majukumu yao.

 

WCF ni mfuko unaoshughulikia fidia kwa wafanyakazi wanaopata madhara yanayotokana na kazi, ikiwemo ajali kazini, magonjwa yatokanayo na kazi na ulemavu unaohusiana na kazi, kwa mujibu wa sheria. Mafunzo hayo yanatarajiwa kusaidia kuongeza uelewa kwa waajiri na maafisa wanaohusika na masuala ya wafanyakazi, ili kuimarisha utekelezaji wa wajibu wa kisheria na kulinda ustawi wa wafanyakazi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.