Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajia kuongoza mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na wenye Ulemavu), Hayati William Vangimembe Lukuvi, yatakayofanyika katika Kijiji cha Idodi mkoani Iringa hii leo Machi 31, 2026.

Kifo cha Lukuvi kilitokea Machi 25, 2026, katika hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Discussion
Reader comments
0 contributions