Skip to main content

KATAVI: WAZIRI MKUU AZINDUA SHULE YA AMALI MGOMBE

Na Daniel Gahu - Katavi.

KATAVI: WAZIRI MKUU AZINDUA SHULE YA AMALI MGOMBE

Na Daniel Gahu - Katavi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Machi 15, 2026 ameweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari Mgombe yenye mkondo wa Amali ya Kihandisi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, katika mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Katavi.

Ujenzi wa shule hiyo unatekelezwa kupitia Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa gharama ya shilingi bilioni 1.694 na hadi sasa umefikia asilimia 99 ya utekelezaji.

Shule hiyo, itatoa mafunzo ya amali katika fani mbalimbali zikiwemo ufundi magari, ufundi bomba, mifumo ya umeme wa jua pamoja na ufundi umeme wa magari, lengo likiwa ni kuwajengea wanafunzi ujuzi wa vitendo utakaowawezesha kujiajiri, kuajiriwa au kuendelea na masomo ya elimu ya juu.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya msingi Inyonga, Dkt. Nchemba ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Katavi kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo, akisema ujenzi wa shule hiyo umefanyika kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.

Amesema, shule za sekondari zenye mkondo wa amali ya kihandisi zimejengwa 103 nchi nzima, na tayari wanafunzi wapo shuleni wakipata elimu inayowawezesha kupata ujuzi wa vitendo sambamba na masomo ya darasani.

Aidha, amesema Mkoa wa Katavi umefanikiwa kupata Hospitali ya Rufaa ya Mkoa pamoja na hospitali mpya tatu zilizojengwa katika kila Halmashauri ya mkoa huo, hatua inayolenga kuboresha huduma za afya na kuwasogezea wananchi huduma hizo karibu zaidi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.