Skip to main content

WAZEE WALIA NA VITENDO VYA UKATILI, UNYANYAPAA KIGOMA

Leo Oktoba Mosi, dunia imeadhimisha ya siku ya Wazee Duniani ikiwa ni siku ya kukumbuka mema na mchango wao katika jamii, Kwa baadhi ya Wazee wa Mkoa wa Kigoma wamesema licha ya kuadhimisha siku hii bado wanatamani kuona jamii ikiendelea kuwajali na kuwalinda kwa kuhakikisha wanapata huduma muhimu ikiwemo huduma bora za afya.

WAZEE WALIA NA VITENDO VYA UKATILI, UNYANYAPAA KIGOMA
Studio Narration JAMBO FM

WAZEE WALIA NA VITENDO VYA UKATILI, UNYANYAPAA KIGOMA

0:00 --:--

Leo Oktoba Mosi, dunia imeadhimisha ya siku ya Wazee Duniani ikiwa ni siku ya kukumbuka mema na mchango wao katika jamii, Kwa baadhi ya Wazee wa Mkoa wa Kigoma wamesema licha ya kuadhimisha siku hii bado wanatamani kuona jamii ikiendelea kuwajali na kuwalinda kwa kuhakikisha wanapata huduma muhimu ikiwemo huduma bora za afya.

Aidha unyanyapaa kwa wazee hawa pamoja na kuwatelekeza wakati wao waliwalea watoto wao na jamii ni mambo wanayoyataja kama changamoto kubwa kwao na kutaka msaada wa serikali na wadau mbalimbali ili waweze kuishi vizuri.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ambayo yamefanyika leo Octoba 1, 2026 mjini Kigoma, Kaimu Mwenyekiti wa baraza la wazee Mkoa wa Kigoma Elias Kwengineza pamoja na mambo mengine amesema licha ya jitihada mbalimbali za Serikali katika kuboresha maisha ya wazee bado sera za kuwalinda wazee zinatakiwa kuangaliwa upya, ikiwemo ulinzi wa wazee na Serikali kuangalia utaratibu mzuri wa kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili

Naye Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kigoma, Bi. Epheta Msiga alisema Serikali wakishirikiana na wadau wa maendeleo wanaendelea kuweka mazingira rafiki ya Wazee kuishi, huku akisisitiza Wazazi wa kizazi cha sasa kutimiza wajibu kwa watoto ili baadae watoto wakishakuwa watu wazima nao waweze kuwatunza wazazi wao kwa upendo

Kwa upande wake Mgeni rasmi kwenye Maadhimisho hayo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Bakari Tambwe alisema inasikitisha kuona baadhi ya Watoto wamekuwa wakiwatelekeza Wazazi wao na kujikuta wanalelewa kwenye vituo vya kulelea Wazee, huku akikemea tabia ya baadhi ya Wananchi wakiona Mtu amekuwa Mzee wanampatia majina yanayoendana na Imani za kishirikina nakupelekea Wazee hao kufanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo kutengwa na Jamii

Maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani Mwaka huu 2026 yamebebwa na Kauli mbiu isemayo Zama za Maisha marefu tuboreshe maisha kwa Wazee

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.