Skip to main content

WAZAZI WASOMESHENI WATOTO DINI KUZUIA MMOMONYOKO WA MAADILI - SHEIKH KWEZI

Na Saada Almasi, Maswa - Simiyu.

WAZAZI WASOMESHENI WATOTO DINI KUZUIA MMOMONYOKO WA MAADILI - SHEIKH KWEZI
Studio Narration JAMBO FM

WAZAZI WASOMESHENI WATOTO DINI KUZUIA MMOMONYOKO WA MAADILI...

0:00 --:--

Na Saada Almasi, Maswa - Simiyu.

Kilio cha mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu kinazidi kukua na wazazi hasa wanawake wakitupiwa jicho kwa kuonekana ndiyo chanzo cha vijana kuwa watukutu na kutofuata misingi ya maisha kwani wao ndiyo mara nyingi huwepo nyumbani pindi ambapo baba anakwenda kutafuta rizki.

Hata hivyo miaka ya hivi karibuni wazazi wote wawili wamekuwa katika jukumu la utafutaji na kuchukua muda wao mwingi zaidi ya kukaa na watoto japokuwa bado mama amebaki kuwa mlezi wa kwanza wa kunyoosha maadili ya mtoto.

Kufuatia suala hilo Sheikh mkuu wa mkoa wa Simiyu amewakutanisha pamoja wazazi wa watoto wanaosoma katika kituo cha kiimani cha dini ya kiislamu Istiqama kijiji cha Malampaka wilayani Maswa mkoani humo na kuzungumza nao juu ya malezi na makuzi ya waoto akiwasihi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwapeleka watoto wao katika masuala ya dini kwani ndiyo mwongozo wa maisha.

“nawapongeza sana akina mama kuwa mstari wa mbele kuwapeleka watoto wenu kupata elimu na ukiangalia wasomi wakubwa duniani wengi wao wameshikwa mkono na mama zao kuwapeleka kupata elimu hayo ni manufaa makubwa kwa sababu muda mwingi mpo nao nyumbani zaidi kuliko baba”amesema Sheikh Kwezi.

“Pamoja na hayo bado mnanyooshewa vidole mtoto akiwa katika njia isiyo sahihi kumbe wanaume tunasahau kuwa jukumu hili si la mama pekee bali wote tunatakiwa kushirikiana na mtoto ukimfundisha quran akaielewa maisha yake pia yamenyooka kwa sababu muda wote itamkumbusha kuwa pamoja na shahada ama astashahada uliyonayo bado kuwa Mungu na wazazi waliokuzaa huyo mtoto hatotenda maovu,” ameongeza Sheikh Kwezi.

Sambamba na hilo Sheikh Kwezi amesisitiza juu ya umuhimu wa kutunza amani ya nchi na kusema kuwa mahali pasipo kuwa na amani hakuna jambo lolote la kimaendeleo litakalo fanyika hivyo wazazi waendeleekuwanasihi watoto ili wapite katika njia sahihi.

Wakitoa maoni yao kuhusiana na malezi baadhi ya wazazi wamesema kuwa mivurugano na migongano kati ya baba na mama ndani ya nyumba ndiyo husababisha maadili mabovu kwa vijana.

“mama anafikisha kwa watoto kile ambacho baba kampatia sasa kama baba anatabia a kukaa vibaya na mama nyumbani hamsikilizi,kipigo kumtia visirani hayohayo ndiyo mama atakayokuja kuwapatia watoto pindi baba atakaokuwa hayupo,"

"Usitegemee mama atawazingatia watoto na kuwa mwema kwao kwa sababu hiyo nachelea kusema wanaume pia tuna mchango mkubwa mama anapokaa kimya kukujibu mume wake tegemea watoto watafikishiwa zile hasira zote,” amesema Khalid Ndile mkazi wa Malampaka

“familia nyingi mama hubaki kuwa mama wa nyumbani baba ndiye mtafutaji kwa hiyo niwashauri tu wamama wenzangu tusikatishe ndoto za watoto wetu kwa kutotimiza wajibu wetu jukumu la malezi ni kubwa na zito yafaa kulitilia maanani wazazi wote wawili”amesema Mwajuma Muhsin mkazi wa Malampaka

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.