Skip to main content

WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUWA KARIBU NA WATOTO

Wazazi na walezi Mkoani Singida wametakiwa kuwa karibu na watoto wao, kuwalea na kuwasimamia katika elimu na maisha, ili kuwakinga na changamoto zinazoweza kuathiri mustakabali wao.

WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUWA KARIBU NA WATOTO
Studio Narration JAMBO FM

WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUWA KARIBU NA WATOTO

0:00 --:--

Wazazi na walezi Mkoani Singida wametakiwa kuwa karibu na watoto wao, kuwalea na kuwasimamia katika elimu na maisha, ili kuwakinga na changamoto zinazoweza kuathiri mustakabali wao.

Akizungumza katika Mahafali ya 18 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Kinyangiri, Wilaya ya Mkalama, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amesema elimu ni msingi wa maisha, hivyo wazazi hawapaswi kuishia kuwapeleka watoto shule, bali wanapaswa kufuatilia mwenendo wao na kushirikiana na walimu katika malezi na maendeleo.

Dendego amesema mtoto asipopata malezi na mwongozo kutoka kwa wazazi na walimu, anaweza kufundishwa na mazingira ya dunia yenye changamoto, akiwataka wahitimu kuepuka makundi mabaya, ulevi, dawa za kulevya na vitendo vinavyoweza kuvuruga ndoto zao.

“Ukichekea mtoto, atafunzwa na ulimwengu, na ulimwengu una mambo mengi mabaya,” amesema Dendego, huku akiwataka wahitimu kutumia elimu, sayansi na teknolojia kujifunza, kujenga maisha yenye mwelekeo na kuwa raia wema wanaopenda amani.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akiwa Kwenye Mahafali ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Kinyangiri iliyopo Wilaya ya Mkalama.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Kinyangiri amesema shule hiyo ina wanafunzi 616 na walimu 29, huku ikiendelea kuimarisha taaluma, nidhamu na michezo. Amesema shilingi milioni 518 zimetumika katika ujenzi wa miundombinu, pamoja na kubainisha changamoto za mabweni, jiko, nyumba za walimu, maabara, maktaba, ukumbi na kompyuta.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wahitimu, Nasra Ramadhan amesema wanafunzi hao walisajiliwa mwaka 2023 wakiwa 194 na sasa wanahitimu 129, huku shule hiyo ikipata ufaulu wa asilimia 100 mwaka 2025. Wahitimu hao wameahidi kuwa raia wema, kutumia elimu waliyoipata kujenga maisha yao na kulitumikia taifa.

Wahitimu wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Kinyangiri wakiwa kwenye Mahafali ya kuhitimu Elimu yao ya Sekondari.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.