Wazazi waislamu wa eneo la Kisesa, Mwanza wametumia siku ya Eid Al-Adha au Eid ya Kuchinja kama darasa la vitendo la kulea watoto wao kimaadili na kiroho.
Siku hii ya sikukuu, inasherekewa kwa wingi na waumini wa dini ya kiislam duniani kote Lakini kwa hapa kisesa wazazi wameamua kutumia siku hii kumkumbusha mtoto jinsi ya kuishi kwa maadili bora na yenye kupendeza katika jamii
Bwana Juma Hassan, ni mkazi wa Kisesa, Amesema kua Eid ya kuchinja ni wakati mzuri wa kuwafundisha watoto maana ya kujitoa na huruma.

“Kila mwaka baada ya swala tunakaa na watoto. Nawafundisha kwa nini tunachinja, na jinsi nyama inavyogawiwa kwa jamaa na maskini. Wanajifunza kutoa tangu wadogo,”
Bi. Aisha Mohamed, ni mama wa watoto watatu, alisema anatumia siku hii kuwaonesha watoto umuhimu wa ushirikiano na usafi.
“Watoto wanashiriki kupanga nyama, kupika na kugawa kwa majirani. Hapo wanajifunza heshima, unyenyekevu na upendo kwa wengine,

Naye Bwana Ibrahim Salum aliongeza kuwa wazazi wanapaswa kutumia Eid ya kuchinja kuwaunganisha watoto na mila na maadili ya kiislamu.
“Watoto wanapoona baba na mama wakifanya kazi pamoja, wanajifunza mshikamano. Hii inajenga familia imara,”
Viongozi wa kidini wa Kisesa wameipongeza hatua hiyo na kuwataka wazazi wengine kutumia sikukuu hii sio tu kwa ajili ya sherehe, bali pia kwa kulea kizazi chenye nidhamu, heshima na woga wa Mungu.
Discussion
Reader comments
0 contributions