Skip to main content

WATUMISHI SABA GEITA WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA

Na Ibrahim Rojala - Geita.

WATUMISHI SABA GEITA WAPANDISHWA  KIZIMBANI KWA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA

Na Ibrahim Rojala - Geita.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita, imewafikisha mahakamani watumishi watatu wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita wakikabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi 48,067,500.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Juni 17, 2026, fedha hizo zilidaiwa kukusanywa kupitia mfumo wa Local Government Revenue Collection Information System (LGRCIS) kwa kutumia mashine za kukusanyia mapato (POS), lakini hazikuwasilishwa kwenye akaunti ya serikali kinyume na taratibu.

Watuhumiwa waliohusika na ubadhirifu huo ni Afisa Umwagiliaji Halmashauri ya  Manispaa ya Geita, Ally Hasan Semfukwe, Afisa Mifugo halmashauri ya Manispaa ya Geita, Edward Cloward na Mkusanya mapato wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Happyness Regnes Mushi.

TAKUKURU pia imewafikisha mahakamani watumishi wanne wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita kwa tuhuma za ubadhirifu wa Shilingi 41,987,607.5 kutoka akaunti ya mirathi ya Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Geita.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watuhumiwa walidaiwa kuwalipa watu wawili ambao hawakuwa na madai ya mirathi ili baadaye warejeshe fedha hizo (kickback) kupitia miamala ya benki na simu.

Watumishi waliohusika na ubadhirifu huo ni Afisa Hesabu Mkuu,Bulemo Yuda Mswaga, Msaidizi wa Hesabu, Mercy Geoffrey Magezi, Mhasibu Baldo Donatus Kafene na William John Mbwambo ambaye ni Dereva.

Kwa mujibu wa taarifa ya TAKUKURU mkoa wa Geita, watuhumumiwa hao walishirikiana na watumishi wengine kutoka idara zingine za serikali  ambao ni Fundi Sanifu kutoka Chuo cha Utafiti wa Dawa Mwanza, Mernad Mernad Mbena na Muuguzi wa hospitali ya Rufaa Bugando, David Thomas Moshy.

Aidha watuhumiwa tajwa wamefikishwa mahakamani Juni 17,2026 na kufunguliwa mashauri manne katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Geita.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.