Skip to main content

WATUMISHI WATAKIWA KUSHIRIKI MICHEZO KULINDA AFYA ZAO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. John Mboya amewataka watumishi wa umma kushiriki michezo na kufanya mazoezi mara kwa mara kwa lengo la kuimarisha afya, kujenga mshikamano na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

WATUMISHI WATAKIWA KUSHIRIKI MICHEZO KULINDA AFYA ZAO
Studio Narration JAMBO FM

WATUMISHI WATAKIWA KUSHIRIKI MICHEZO KULINDA AFYA ZAO

0:00 --:--

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. John Mboya amewataka watumishi wa umma kushiriki michezo na kufanya mazoezi mara kwa mara kwa lengo la kuimarisha afya, kujenga mshikamano na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ametoa kauli hiyo alipokutana na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa huo wanaoshiriki Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayofanyika Mkoani Kilimanjaro.

Amesema michezo ni sehemu muhimu ya maisha ya mtumishi wa umma kwa kuwa, pamoja na kuimarisha afya ya mwili, husaidia kujenga mahusiano mazuri na mshikamano miongoni mwa watumishi, hali inayoweza kuchangia ufanisi katika utendaji wa kazi.

Katika kikao hicho, Dkt. Mboya amewataka washiriki kutoka Mkoa wa Tabora kuonesha uwezo, nidhamu na ushindani wa kweli katika mashindano hayo huku wakihakikisha wanalinda heshima na taswira ya Mkoa.

Aidha, amewasisitiza kuzingatia kanuni na taratibu za mashindano, kushirikiana kama timu na kuwa mabalozi wazuri wa Mkoa wa Tabora ndani na nje ya viwanja.

Mashindano ya SHIMIWI 2026 yanafanyika Mkoani Kilimanjaro kuanzia Septemba 19 hadi Oktoba 7, 2026, yakiwa na kaulimbiu “Tupo Tayari kwa AFCON 2027”, huku ufunguzi rasmi wa mashindano hayo ukitarajiwa kufanyika kesho Septemba 25, 2026.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.