Skip to main content

WATUMISHI WAANZILISHI WA MIGOGORO YA ARDHI KUKIONA, RC SENDIGA ATOA ONYO

Na Afarah Suleiman, Babati - Manyara.

WATUMISHI WAANZILISHI WA MIGOGORO YA ARDHI KUKIONA, RC SENDIGA ATOA ONYO
Studio Narration JAMBO FM

WATUMISHI WAANZILISHI WA MIGOGORO YA ARDHI KUKIONA, RC SENDI...

0:00 --:--

Na Afarah Suleiman, Babati - Manyara.

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amesema atawachukulia hatua ikiwemo kuwapeleka Mahakamani watumishi ambao wanasabisha migogoro ya ardhi katika eneo la Makatanini wilayani Babati mkoani Manyara.

Sendiga amesema hayo katika kikao Cha Baraza la madiwani la halmashauri ya mji wa Babati,na kukemea vitendo vya baadhi ya watumishi wa serikali wanaoshikilia viwanja na kuwambia wananchi vimechukuliwa kwa maslahi yao binafsi.

Katika hatua nyingine Sendinga amelitaka Baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Babati kutoweka vikwazo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza baada ya kufunguliwa kwa geti la Mamire wilayani Babati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati, Yona Wawo amesema amesema Baraza la madiwani limepitisha na kukubali uwekezaji unaotarajiwa kufanywa na Shirika la NSSSF katika halmshauri ya mji wa Babati.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.