Skip to main content

WATUMISHI WA UMMA WASAIDIENI WAWEKEZAJI KUPATA VIBALI KWA WAKATI - CP HAMDUNI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni amewataka watumishi wa umma kusaidia wawekezaji wa miradi ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kupata vibali vya kisheria kwa wakati.

WATUMISHI WA UMMA WASAIDIENI WAWEKEZAJI KUPATA VIBALI KWA WAKATI - CP HAMDUNI
Studio Narration JAMBO FM

WATUMISHI WA UMMA WASAIDIENI WAWEKEZAJI KUPATA VIBALI KWA WA...

0:00 --:--

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni amewataka watumishi wa umma kusaidia wawekezaji wa miradi ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kupata vibali vya kisheria kwa wakati.

Agizo hilo amelitoa leo tarehe 19 Oktoba, 2026 wakati akikagua ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza chakula cha samaki cha kampuni ya The Big Best Company Limited chenye thamani ya Tshs. Bilioni 20 na shamba la vizimba Kayenze, Magu.

Mkuu wa Mkoa amesikitishwa na kutowajibika kwa baadhi ya watendaji na amewataka watumishi wote kuhakikisha wanawajibika ipasavyo, la sivyo atakaekiuka atachukuliwa hatua za kinidhamu.

“Watendaji kutoka wizara ya Mifugo na Uvuvi, Idara pamoja na wadau wote msaidieni mwekezaji katika kupata vibali vyote vikiwemo ardhi na uhifadhi wa mazingira kabla ya kuendelea na kazi ya ujenzi wa mabwawa ya kukuzia vifaranga vya samaki na upanuzi wa mradi huu kwa ujumla kinyume na sheria," amesema.

Amesema, kiwanda hicho na mashamba ya vizimba 1000 vinavyojengwa vita chechemua uchumi wa wafugaji wa Magu na Mwanza kwa ujumla, na kukuza ushoroba wa teknolojia ya kisasa ya ufugaji ambapo vitaleta mapinduzi ya upatikanaji wa chakula cha samaki kwa wafugaji.

“Nichukue wasaa huu kuwapongeza kwa uwekezaji mkubwa, kiwanda hiki kitachchemua uchumi wa wananchi wa Magu na kitaongeza upatikanaji wa chakula kwa wafugaji wote kwani zaidi ya tani 35,000 zitazalishwa kwa siku,” amesema.

Kadhalika amewahimiza wananchi kuchangamkia fursa za ajira kupitia uwekezaji huo na kuwa waaminifu ili pande zote mbili, mwekezaji na jamii, zinufaike.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.