Skip to main content

WATUMISHI WA UMMA SINGIDA WAAGIZWA KUTEKELEZA SERA KWA VITENDO

Watumishi wa Umma katika Manispaa ya Singida wametakiwa kutafsiri sera, misingi na malengo ya Serikali kwa vitendo ili kuwaletea maendeleo wananchi katika maeneo yao.

WATUMISHI WA UMMA SINGIDA WAAGIZWA KUTEKELEZA SERA KWA VITENDO
Studio Narration JAMBO FM

WATUMISHI WA UMMA SINGIDA WAAGIZWA KUTEKELEZA SERA KWA VITEN...

0:00 --:--

Watumishi wa Umma katika Manispaa ya Singida wametakiwa kutafsiri sera, misingi na malengo ya Serikali kwa vitendo ili kuwaletea maendeleo wananchi katika maeneo yao.

Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego wakati wa majumuisho ya ziara yake katika Wilaya ya Singida yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Uhasibu (TIA),Mjini Singida.

Akizungumza katika kikao hicho, Dendego amewataka watumishi wa umma Wilayani Singida kutafsiri sera, sheria na miongozo ya Serikali kwa vitendo ili kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma.

"Sera zipo nyingi na nzuri, lakini kama hazitatafsiriwa kwa vitendo, wananchi hawatanufaika. Nataka kila mtumishi awe balozi wa utekelezaji wa sera katika eneo lake la kazi," amesema Dendego.Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe amesema kuwa maagizo na maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa atayatekeleza haraka iwezekanavyo kwa kushirikiana na watumishi wote

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.