Skip to main content

WATUMISHI SINGIDA WAPATIWA ELIMU BIMA YA AFYA

Watumishi wa Umma kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wamepatiwa elimu kuhusu Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) ili kuwawezesha kuwa mabalozi wa kuhamasisha jamii kujiunga na mfumo huo.

WATUMISHI SINGIDA WAPATIWA ELIMU BIMA YA AFYA
Studio Narration JAMBO FM

WATUMISHI SINGIDA WAPATIWA ELIMU BIMA YA AFYA

0:00 --:--

Watumishi wa Umma kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wamepatiwa elimu kuhusu Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) ili kuwawezesha kuwa mabalozi wa kuhamasisha jamii kujiunga na mfumo huo.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Rodrick Mpogolo, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwapa watumishi uelewa wa kutosha juu ya Bima ya Afya kwa lengo la kwenda kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wake kwa kila mmoja.

Mpogolo amesema bima hiyo inawahakikishia wananchi usalama wa afya kwa matibabu ya uhakika na bei nafuu wakati wote ikiwemo wakati wa dharura.

Aidha, amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi Octoba 22,2026 katika kituo cha Sokoine kilichopo Manispaa ya Singida, ambapo utafanyika uzinduzi rasmi wa Bima ya Afya kwa Wote.

Amesema uzinduzi huo utatoa fursa kwa wananchi kupata elimu ya kina, kutoa maoni, kupata matibabu bure pamoja na kusajiliwa ili kuwezesha kila familia kuwa na ulinzi wa kiafya.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.