Skip to main content

WATUMISHI KATAVI WAHIMIZWA KUZINGATIA UADILIFU UTOAJI HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Na Daniel Gahu - Katavi.

WATUMISHI KATAVI WAHIMIZWA KUZINGATIA UADILIFU UTOAJI HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Na Daniel Gahu - Katavi.

Kufuatia changamoto za utoaji wa huduma kwa wananchi, baadhi ya watoa huduma kukumbana na tuhuma za utendaji mbovu wa kazi, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Florence Chrisant, amewahimiza watumishi wa umma kuongeza uwajibikaji na weledi katika utoaji wa huduma kwa wananchi, ili kuhakikisha huduma zinakuwa bora, zenye ufanisi na zinazokidhi matarajio ya jamii.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya Mobile Clinic yenye lengo la kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi pamoja na Manispaa ya Mpanda kuhusu matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa e-Utendaji (PEPMIS), Chrisant alisema ni muhimu kila mtumishi kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu kuanzia ngazi ya chini, ili kuepusha kero kufika katika ngazi za juu za uongozi.

“Ni wajibu wa kila mtumishi kuhakikisha anatimiza majukumu yake ipasavyo katika nafasi yake, ili kudhibiti changamoto mapema kabla hazijawa kubwa na kufikishwa kwa viongozi wa juu,” alisisitiza.

Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, yakilenga kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kupitia matumizi sahihi ya mfumo wa e-Utendaji.

Kwa upande wake, Afisa kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Kassim Dihenga, amesema kuwa matumizi ya mfumo wa e-Utendaji (PEPMIS) yana manufaa makubwa ikiwemo kuongeza uwazi, kurahisisha ufuatiliaji wa utendaji wa watumishi, pamoja na kuimarisha uwajibikaji serikalini.

Ameongeza kuwa mfumo huo unasaidia kupima utendaji kazi kwa usahihi, kuweka kumbukumbu za kazi zinazotekelezwa, na kutoa fursa kwa taasisi za umma kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.