Skip to main content

WATUMIAJI VYOMBO VYA MOTO KANDA YA ZIWA WAHIMIZWA UMUHIMU WA KUKATA BIMA

Watumiaji wa vyombo vya moto nchini Tanzania wametakiwa kuelewa umuhimu wa kuwa na bima sahihi, si tu kwa ajili ya kufuata sheria bali pia kujilinda wao binafsi pamoja na mali zao dhidi ya madhara ya ajali.

WATUMIAJI VYOMBO VYA MOTO KANDA YA ZIWA WAHIMIZWA UMUHIMU WA KUKATA BIMA
Studio Narration JAMBO FM

WATUMIAJI VYOMBO VYA MOTO KANDA YA ZIWA WAHIMIZWA UMUHIMU WA...

0:00 --:--

Watumiaji wa vyombo vya moto nchini Tanzania wametakiwa kuelewa umuhimu wa kuwa na bima sahihi, si tu kwa ajili ya kufuata sheria bali pia kujilinda wao binafsi pamoja na mali zao dhidi ya madhara ya ajali.

 Hayo yameelezwa na wataalamu wa bima wakibainisha kuwa ongezeko la vyombo vya moto barabarani linaenda sambamba na kuongezeka kwa ajali, hali inayohitaji tahadhari zaidi ikiwemo matumizi sahihi ya bima.

Halfan Isango Afisa Ubora na mtaalamu wa Bima kutoka Mamlaka  ya Bima Tanzania, ofisi za kanda  ya ziwa  amesema kuwa, kuna aina kuu tatu za bima kwa vyombo vya moto.

Amesema, bima kubwa, ya kati na ndogo, kila moja ikiwa na wigo tofauti wa kinga kulingana na mahitaji ya mtumiaji. Aidha, wataalamu wanaeleza kuwa bima hutoa kinga si kwa dereva pekee bali pia kwa abiria na watu wengine wanaoweza kuathirika endapo ajali itatokea.

Oyuke Faustine, Meneja wa TIRA kanda ya ziwa ameongeza kuwa katika tukio la ajali, fidia hutolewa kulingana na aina ya bima iliyochukuliwa, ikijumuisha gharama za matibabu, fidia ya ulemavu wa kudumu au malipo kwa familia endapo kifo kitatokea.

 Sambamba na hilo, mamlaka hiyo imeendelea kusisitiza jukumu lake la kulinda haki za watumiaji wa bima pamoja na kusimamia kampuni za bima ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa weledi na haki kwa wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.