Skip to main content

WATU YAZINDULIWA RASMI SHINYANGA, MISIBA 19 KUTUMIA MILIONI 80

Kikundi cha Wanashinyanga Tusaidiane (WATU), chenye jumla ya wanachama 792 katika Manispaa ya Shinyanga, kimezinduliwa rasmi kwa lengo la kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama wake, hususan katika kipindi cha misiba na changamoto nyingine za kijamii.

WATU YAZINDULIWA RASMI SHINYANGA, MISIBA 19 KUTUMIA MILIONI 80
Studio Narration JAMBO FM

WATU YAZINDULIWA RASMI SHINYANGA, MISIBA 19 KUTUMIA MILIONI...

0:00 --:--

Kikundi cha Wanashinyanga Tusaidiane (WATU), chenye jumla ya wanachama 792 katika Manispaa ya Shinyanga, kimezinduliwa rasmi kwa lengo la kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama wake, hususan katika kipindi cha misiba na changamoto nyingine za kijamii.

VIONGOZI KATIKA KIUKUNDI CHA WATU WAKIKATA KEKI KUASHIRIA MWANZO MPYA WA KIKUNDI HICHO

Hafla ya uzinduzi imefanyika leo, Oktoba 14, 2026, katika Ukumbi wa Lyakale, uliopo ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, na kuzinduliwa na meya wa Manispaa ya Shinyanga Salumu Kitumbo.

MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA SHINYANGA SALUM KITUMBO

Akizungumza katika hafla hiyo, Kitumbo amesema kuanzishwa kwa kikundi hicho ni hatua muhimu katika kuimarisha mshikamano wa kijamii na kusaidiana wakati wa changamoto, akisisitiza kuwa umoja ni nguzo muhimu katika kukabiliana na nyakati za majonzi.

Aidha, amekishauri kikundi hicho kupanua wigo wa huduma zake kwa kujumuisha shughuli za kijamii katika nyakati za furaha, zikiwemo sherehe, ili kuongeza manufaa kwa wanachama wake.

KATIBU WA KIKUNDI HICHO TINNA KESSY

Kwa upande wake, Katibu wa kikundi hicho, Tinna Kessy, akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, amesema kuwa katika kipindi cha miezi mitano tangu kuanzishwa kwake, kikundi hicho kimeshiriki kusaidia misiba 19 kwa jumla ya shilingi milioni 80.

Hata hivyo, Kessy amebainisha kuwa udanganyifu unaohusiana na taarifa za misiba ni miongoni mwa changamoto zinazokikabili kikundi hicho, hali inayohitaji kuwepo kwa mifumo madhubuti ya uthibitishaji wa taarifa ili kuhakikisha misaada inawafikia walengwa halali.

Baadhi ya wanachama waliohudhuria hafla hiyo wamependekeza kuboreshwa kwa shelia na taratibu kwalengo la kuweka misingi imara ya kiutendaji , kuimarisha uwajibikaji, sambamba na kudhibiti vitendo vya udanganyifu.

Kikundi cha Wanashinyanga Tusaidiane (WATU) kilianzishwa mwezi Machi mwaka 2026 kikiwa na wanachama 380, lakini idadi hiyo imeongezeka na kufikia wanachama 792 kwa sasa, huku kikilenga kuendelea kuongeza wanachama na kuimarisha huduma zake kwa jamii.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.