Skip to main content

WATU TISA WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA NDEGE

Watu tisa wamepoteza maisha, baada ya ndege ndogo ya abiria aina ya Learjet 60 kuanguka ghafla katika makazi ya watu, huko Palm Beach County, Florida Kusini nchini Marekani.

WATU TISA WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA NDEGE
Studio Narration JAMBO FM

WATU TISA WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA NDEGE

0:00 --:--

Watu tisa wamepoteza maisha, baada ya ndege ndogo ya abiria aina ya Learjet 60 kuanguka ghafla katika makazi ya watu, huko Palm Beach County, Florida Kusini nchini Marekani.

Kwa mujibu wa Waziri wa Uchukuzi wa Marekani, Sean Duffy, ndege hiyo ilidunda kwa pua na kulipuka moto, tukio lililokaribia kugonga nyumba za raia mita chache kabla ya kuanguka karibu na barabara kuu Novemba 1, 2026.

Duffy alithibitisha kupitia mtandao wa X kuwa ajali hiyo ilitokea saa 12:50 jioni na akaitaja kama "mkasa wa kutisha." Alieleza kuwa abiria wote tisa waliokuwa ndani ya ndege hiyo wamefariki dunia.

CHANZO CHA SAFARI:

Taarifa za awali kutoka Shirika la Usafiri wa Anga la Shirikisho (FAA) zinaonesha kuwa ndege hiyo ilikuwa imetoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Austin-Bergstrom, Texas, na ilikuwa njiani kuelekea Bahamas.

Msemaji wa uwanja huo, Jim Reynolds, alithibitisha kuwa ilikuwa ni ndege binafsi na kusema, "Huu ni msiba mkubwa kabisa," huku akisema bado hawana taarifa kamili za abiria waliokuwa ndani.

UCHUNGUZI WAANZA:

FAA imetangaza kutuma timu maalum ya wataalamu kushirikiana na Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri (NTSB) kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.

Hadi sasa, haijajulikana kama kuna majeruhi au vifo kwa watu waliokuwa ardhini wakati wa ajali hiyo, na chanzo halisi cha ndege kuanguka bado hakijabainika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.