Skip to main content

WATU 12 WAFARIKI AJALI YA MLIMA SEKENKE, ASKARI POLISI 5 NA MAHABUSU 7

Watu 12 wamefariki dunia, wakiwemo askari Polisi watano na mahabusu saba, katika ajali iliyohusisha magari mawili eneo la Mlima Sekenke Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

WATU 12 WAFARIKI AJALI YA MLIMA SEKENKE, ASKARI POLISI 5 NA MAHABUSU 7
Studio Narration JAMBO FM

WATU 12 WAFARIKI AJALI YA MLIMA SEKENKE, ASKARI POLISI 5 NA...

0:00 --:--

Watu 12 wamefariki dunia, wakiwemo askari Polisi watano na mahabusu saba, katika ajali iliyohusisha magari mawili eneo la Mlima Sekenke Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Amon Kakwale, amesema ajali hiyo imetokea Septemba 21,2026 majira ya saa 2:00 asubuhi, baada ya gari la tank la mafuta lenye namba RAF 245X na tela lake lenye namba RL 4255 lililokuwa na mwelekeo wa kutoka Singida kwenda Tabora kugonga gari ndogo yenye namba PT 1982 aina ya Toyota Land Cruiser, mali ya Jeshi la Polisi.

Amesema gari hilo la Polisi lilikuwa limewabeba mahabusu 8 na askari Polisi 5 akiwemo afisa mmoja wa polisi ambae ni Mkuu wa Kituo waliokuwa wakielekea Mahakama ya Kiomboi ambapo watu 12 wamepoteza maisha, huku watu wawili wakijeruhiwa, akiwemo mahabusu mmoja na dereva wa lori hilo.

“Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari la tank kushindwa kulimudu gari hilo na kuelekea upande wa kulia na hivyo kuligonga gari hilo uso kwa uso,” amesema Kamanda Kakwale.

Kwa mujibu wa Kamanda Kakwale Jeshi la Polisi limeanza taratibu za kuandaa miili ya askari hao ambayo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa ili kusafirishwa kwenda katika maeneo yao waliyozaliwa kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Kamanda Kakwale ametoa rai kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani pamoja na kufuata alama za barabarani, akitolea mfano eneo la Mlima Sekenke.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.