Skip to main content

WATU 1,066 WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI ZA BARABARANI NCHINI

Jumla ya Watu 1,066 wamepoteza maisha kwa ajali za barabarani katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025 ikilinganishwa na Watu 1,275 waliopoteza maisha katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2025/2026.

WATU 1,066 WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI ZA BARABARANI NCHINI
Studio Narration JAMBO FM

WATU 1,066 WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI ZA BARABARANI NCHINI

0:00 --:--

Jumla ya Watu 1,066 wamepoteza maisha kwa ajali za barabarani katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025 ikilinganishwa na Watu 1,275 waliopoteza maisha katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2025/2026.

Hayo yamebainishwa hii leo Mei 25, 2026 na Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo bungeni jijini Dodoma.

Amesema, “takwimu zinaonesha kuwa matukio ya usalama barabarani yaliyotolewa taarifa katika vituo vya Polisi Nchini yamepungua kutoka 1,322 katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025 na kufikia 1,233 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2025/2026 ikiwa ni upungufu wa asilimia 16.4.”

Katambi amesema katika ajali hizo, Watu 1,869 walijeruhiwa ikilinganishwa na Watu 2,278 waliojeruhiwa kwa kipindi kama hicho mwaka 2024/2025.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.