Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.
Watoto wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Zaqahana kilichopo mtaa wa Iponya kata ya Kagongwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga wapo mbioni kuondolewa katika nyumba wanayoishi baada ya mkataba kuisha.
Hayo yamebainishwa na watoto hao katika risala yao mbele ya mgeni rasmi wakati wa Ufunguzi wa jengo lao la kuishi watoto hao ambalo halijakamilika lililopo mtaa wa Iponya kata ya Kagongwa.
“Ndugu mgeni rasmi tunaiomba serikali wewe Pamoja na wadau wengine mtushike mkono ili tuweze kukamilisha ujenzi wa nyuma ya kuishi kwani kwasasa tunaishi kwenye nyuma ya kupanga na mkataba wa kuishi katika nyumba hiyo unaisha Julai 30 mwaka huu hivyo hatuna sehemu nyingine ya Kwenda,” wamesema watoto hao kupitia risala.

Sambamba hayo watoto hao wamesema kuwa wanakailiwa na changamoto nyingi katikka kituo hicho ikiwemo ukosefu wa usafiri kwa ajili ya kuwasafirisha watoto sehemu mbalimbali kama vile hospitali Pamoja gharama za kila siku za chakula matibabu pamoja mishahara wa walezi katika kituo hicho.
“Sambamba na hayo tunakailiwa na ukosefu wa gari kwa ajili ya kusarisha watoto Kwenda sehemu mbalimbali kama hospitali Pamoja na gharama kubwa ya kila siku ya chakula na ukosefu wa mishahara kwa walezi ambao wanatulea na kutusimamia,” wameongeza watoto hao.

Naye mkurugenzi wa kituo hicho Zakia Mwambiko amesema kuwa kituo hicho kwa sasa kinahudumia watoto wapatao 60 na jengo jipya ambalo linahitaji ukamilishaji lina vyumba 30 na matundu ya vyoo nane, vinne vya wavulana na vine vya wasichana.
“Kituo chetu kwasasa kinahudumia watoto wapatao 30 na jengo letu ambalo tunaendelea na ujenzi lia vyuma 30 na vyoo 8,vinne vya wavulana na vinne vya wasichana,hivyo likikamilika litawasaidia watoto hawa kupata makazi ya kudumu yenye ulinzi na usalama,” amesema Bi Mwambiko.

Kwa upande wake Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Biliwayo kutoka kampuni ya ArrowTech amesema kuwa kupitia ofisi yao watatoa mbao 400 za kupaulia jengo hilo Pamoja na mabati huku akihaidi kusimamia hatua zote za kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ili likamilike kwa wakati watoto hao waweze kuhamia haraka iwezekanavyo.
“Mimi pamoja na wafanyakazi wenzangu,kupitia kampuni yetu tutatoa mbao 400 na maati kwa ajili ya kupaua jengo hili,na kuna fedha ambazo tumeanza kutuma kwa mkurugenzi ili zisaidie katika majukumu mbali mbali ya kituo,lengo letu tunahitaji jengo hili liishe haraka hata kabla ya Julai 30 ili watoto wetu waweze kuhamia,” amesema Biliwayo.
Discussion
Reader comments
0 contributions