Skip to main content

WATOTO WAWILI KATI YA 100 NCHINI HUZALIWA NA MATATIZO YA MOYO - DKT. KISENGE

Na Ibrahim Rojala - Geita.

WATOTO WAWILI KATI YA 100 NCHINI HUZALIWA NA MATATIZO YA MOYO - DKT. KISENGE

Na Ibrahim Rojala - Geita.

Watoto wawili kati ya 100 wanaozaliwa nchini huzaliwa wakiwa na matatizo ya moyo, wakati watoto 13,000 kati ya vizazi zaidi ya milioni mbili huzaliwa wakiwa na matatizo ya moyo na mishipa ya damu na kati yao 4,000 huhitaji  upasuaji wa haraka au kuzibwa matundu katika moyo haraka ili kuokoa maisha yao.

Takwimu hizo, zimetolewa Agosti 14, 2026 na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge akiwa mkoani Geita wakati wa kusainiwa kwa Makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati wa miaka mitatu kati ya Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wenye lengo la kusaidia upatikanaji wa huduma za upasuaji maalumu wa moyo kwa watoto 300 nchini Tanzania kwa gaharama yashilingi bilioni 1.2.

 Dkt Kisengi ameongeza kuwa Serikali imekuwa ikigharamia asilimia 70 ya matibabu ya watoto hao wakatoi asilimia 30 zilizobaki zikitegemea ufadhili kutoka kwa wadau  mbalimbali na kuelezakuwa watoto wengi wanaokabiliwa na matatizo ya magonjwa ya moyo ni kutoka katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Akizungumza kuhusu makubaliano kati ya GGML na JKCI Dkt.  Kisenge, amebainisha kuwa hatua hiyo  itawezesha watoto wengi zaidi wanaohitaji huduma maalumu za matibabu ya moyo kupata matibabu na kuishukuru  Kampuni  ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita kwa uamuzi wa kufadhili matibabu hayo.

“Kwa familia nyingi, gharama za matibabu maalumu ya moyo zinaweza kuwa kikwazo kikubwa kinachomzuia mtoto kupata huduma anayohitaji kwa haraka,ushirikiano huu utatuwezesha kuwafikia watoto wengi zaidi wanaohitaji matibabu, huku tukiimarisha juhudi zetu katika kinga, utambuzi wa mapema na kuongeza uelewa kuhusu afya ya moyo na mishipa ya damu,tunaishukuru GGML kwa kuendelea kushirikiana  nasi na kuwekeza katika afya ya Watanzania,’’ amesema Dkt. Kisenge.

Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Ashraf Suryaningrat, amesema ushirikiano huo unaonesha dhamira ya kampuni ya kushirikiana na taasisi za kitaifa katika kukabiliana na mahitaji muhimu ya huduma za afya na kuchangia katika kuboresha maisha ya Watanzania.

“Nyuma ya kila mtoto anayehitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo, kuna familia yenye matumaini ya kumuona mtoto wao akipona, akikua na kutimiza ndoto na uwezo wake. Kupitia ushirikiano huu na JKCI, tunasaidia kuyageuza matumaini hayo kuwa uhalisia kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma maalumu za matibabu ya moyo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.”

Nae Meneja Mwandamizi wa Masuala ya Uendelevu na Uhusiano wa Jamii katika Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Gilbert Mworia, amefafanua kuwa makubaliano hayo yatawezesha watoto 100 kupata Huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo kila mwaka ndani ya miaka mitatu ya Ushirikiano kati ya GGML na JKCI.

‘Mchango wetu ni wa milioni 400 kwa kila mwaka,kwa miaka mitatu ambayo itakuwa  ni bilioni moja na milioni 200 kwahiyo kwa niaba ya Kampuni ya Geita Gold Mine Limited nipende kuwashukuru sana wenzetu wa Jakaya Kikwete Cardiac Institute kwa kukubali kufanya kazi na sisi na kukubali vile vile kupokea mchango wetu ili kwenda kuwezesha tiba na Huduma kwa watoto wenye mahitaji nchini’,’ amesema Mworia.

Chini ya Hati ya Makubaliano (MoU), GGML itatoa msaada wa kifedha kugharamia upasuaji wa moyo kwa watoto 100 kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitatu, ikiwa ni uwekezaji wa TZS milioni 400 kwa mwaka na hivyo kufikia uwekezaji unaotarajiwa wa jumla ya TZS Bilioni 1.2 katika kipindi chote cha miaka mitatu.

Ushirikiano ni sehemu ya uendelezaji wa msaada ambao Kampuni ya GGML imekuwa ikiutoa katika huduma za matibabu ya moyo kwa watoto tangu Novemba 2024 ambapo GGML imekuwa ikishirikiana na JKCI pamoja na wadau wa sekta ya afya kusaidia kupunguza pengo la gharama za matibabu linalozikabili familia zenye uhitaji,mnamo mwaka 2025, Kampuni ilitoa shilingi milioni 56, ambazo zilisaidia kugharamia upasuaji wa moyo wa kuokoa maisha kwa watoto 14.

Aidha, Ushirikiano na JKCI ni sehemu ya mchango mpana wa GGML katika kuboresha afya na ustawi wa Watanzania, unaojumuisha huduma maalumu za matibabu, miundombinu ya afya, kinga dhidi ya magonjwa, elimu ya afya kwa jamii pamoja na mipango inayolenga kuwafikia wananchi katika maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya.

Mchango wa GGML katika sekta ya afya pia unajumuisha juhudi za kitaifa za kukabiliana na VVU na UKIMWI kupitia GGM Kili Challenge, ambayo kwa zaidi ya miongo miwili imekuwa ikihamasisha sekta binafsi, Serikali, washirika wa maendeleo na jamii kuchangisha fedha na kuongeza uelewa kwa ajili ya kusaidia programu za kinga, matibabu na huduma kwa watu walioathiriwa na VVU na UKIMWI.

Hivyo, ushirikiano na JKCI unaongezta wigo mwingine muhimu katika juhudi hizi kwa kuunganisha msaada wa GGML katika huduma za kinga na afya ya jamii na upatikanaji mpana zaidi wa huduma za matibabu ya kibingwa kwa watoto kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.