Skip to main content

WATOTO WATATU WAKUTWA WAMEFARIKI NDANI YA GARI CHALINZE

Watoto watatu, Masoud Mwema (9), Mikidadi Halfani (4) na Murath Mbaraka (4), wamekutwa wamefariki ndani ya gari katika Kijiji cha Lamboni, kilichopo Kata ya Lugoba, Wilayani Chalinze Mkoani Pwani.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani humo imeeleza kuwa ni kwamba tukio hilo limetokea Julai 9, 2026 majira ya saa 2 asubuhi, baada ya kupokea taarifa ya kupotea kwa Watoto hao watatu, wakazi wa Kijiji cha Lamboni, Kata ya Lugoba.

Inaarifiwa kuwa, Polisi kwa kushirikiana na Wananchi walianza kuwatafuta Watoto hao kuanzia Julai 9 hadi 10, 2026 majira ya saa 7:30 usiku, ambapo Mwanafunzi Lilahi Mbezi Mgaza (19) aliwaona Watoto hao wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Carina Ti lenye namba za usajili T 116 CJV.

Lilahi alitoa taarifa kwa Mohamed Said Muzumba, ambaye ni mmiliki wa nyumba hiyo na baadaye taarifa ziliwasilishwa kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani.

Uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea na miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Msoga, Chalinze.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.