Na Saulo Stephen - Singida.
Jumla ya watoto 832,210 wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya polio, katika awamu ya pili ya zoezi hilo kwenye vituo vya utoaji chanjo 304 Mkoani Singida.
Akizungumzia kuhusu zoezi hilo lililoanza Mei 7 na likitarajiwa kukamilika Mei 10, 2026, Mratibu wa chanjo mkoa wa Singida, Habibu Saidi Mwinory amesema vifaa vyote muhimu vikiwemo chanjo, mabango, vipeperushi na vifaa vya utambuzi vimesambazwa katika vituo vyote vya huduma ambapo zoezi hilo linaendelea mkoani humo.

"Tayari timu ya watoa huduma 1,115 katika halmashauri zote saba, za mkoa wa Singida wakiwemo watoa huduma, watunza kumbukumbu na wahamasishaji walipatiwa mafunzo maalum ambayo yanawasaidia kuhakikisha zoezi linaendeshwa kwa ufanisi," alisema.
Aidha, Mwinory mebainisha kuwa katika awamu ya kwanza ya utoaji wa chanjo ya Polio iliyofanyika Machi 24–27, 2026, mkoa wa Singida, ulifanikiwa kuvuka lengo la Utoaji wa chanjo hiyo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick amesema, utekelezaji wa kampeni hiyo unafanyika kwa ufanisi katika halmashauri zote saba, huku akitoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo hiyo muhimu kwa wakati.
Awali, akiongea kuhusu kampeni ya utoaji wa chanjo ya polio Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Otilia Gowelle amesema, kampeni hiyo inalenga kuwafikia watoto 8,013,525 katika mikoa saba, baada ya mafanikio yaliyoonekana katika awamu ya kwanza.

Discussion
Reader comments
0 contributions