Na Irene Kishiwa - Shinyanga.
Jumla ya Watoto 781,186 wanatarajiwa kupata chanjo ya polio dhidi ya ugongwa wa kupooza baada ya utafiti uliofanywa kubaini maji taka kutoka Mwanza kuwa na vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa kupooza kwa watoto chini ya miaka 10.
Akifungua mafunzo ya Kampeni ya Chanjo hiyo kwa Waandishi wa Habari, Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Yudas Ndungie amesema Serikali imechua hatua hiyo ya mapema, ili kuzuia madhara makubwa yasitokee kwa watoto.

Amesema, chanjo hiyo itatolewa katika Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga ambapo kwa Ushetu watatoa chanjo kwa Watoto 148,557 Kahama Manispaa, 145,820, Msalaa Watoto 138,172, Kishapu watoto 120,01, Shinyanga Vijiji 160,428 na Manispaa ya Shinyanga 62,196.
"Chanjo hiyo Kitaifa itazinduliwa rasmi Mkoani Mwanza ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Waziri wa Afya dokta Dorothy Gwajima na kwa Mkoa wa Shinyanga chanjo hiyo itazinduliwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mboni Mhita na itaanza
rasmi march 24 hadi 27,2026 itakuwa ya nyumba kwa nyumba na itahusu watoto wote walio na umri wa mwaka 0 mpaka 10," alisema dokta Ndungile.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, idara ya kinga na elimu lakini pia muhamasihaji wa kampeni hiyo kwa Mkoa wa Shinyanga Anne Shuma
amesema kampeni kama hii iliwahi kufanyika mwaka 2023 kwa watoto na Serikali imeamua kuirudia baada ya kuonekana kwa vimelea hivyo hatari zaidi kwa watoto kutokana na namna ambavyo wanaweza kujikinga tofauti na
watu wazima.
"Chanjo hii ni salama na haina madhara mtoto anaweza kupata chanjo hiyo leo na kesho akapata tena na itatolewa kwa matone na sio kwa sindano na itatolewa bila malipo na kila mtoto atakae pata chanjo hii umewekwa
utaratibu wa kumuwekea alama katika kidole ili ajulikane kuwa amepata chanjo tayari," alisema.

Naye Mratibu wa Elimu ya Afya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Moses Mwita amebainisha viashiria vya ugojwa huo wa kupooza kwa watoto kuwa ni pamoja na kulemaa ghafla, kulegea viungo,kukosa nguvu na kushindwa kukaa na kuwataka wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika utoaji wa chanjo hiyo kwa watoto wao kutokana na ugonjwa huo kutokuwa na tiba.
Aidha chanjo hiyo pia itatolewa katika Mikoa ya Singida, Tabora, Simiyu, Mwanza, Mara na Geita ambayo iko kwenye hatari ya kuweza kusambaa kwa vimelea hivyo vya ugonjwa wa kupooza kwa watoto.
Discussion
Reader comments
0 contributions