Na Saulo Stephen - Singida.
Serikali kwa kushirikiana na taasisi ya Vision Care, Wizara ya Afya pamoja na TAMISEMI, imepanga kuendesha kliniki kubwa ya macho itakayowanufaisha watoto wapatao elfu 40 mkoani Singida.
Huduma zitakazotolewa katika kliniki hiyo ni pamoja na utoaji wa miwani, dawa pamoja na upasuaji wa macho. Kambi hiyo ya matibabu inatarajiwa kufanyika kuanzia Mei 11 hadi 22, mwaka 2026.
Akizindua mafunzo maalum kwa wakuu wa shule katika Wilaya ya Singida, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Victorina Ludovic amesema kuwa takribani asilimia 80 ya matatizo ya upofu yanaweza kutibika, endapo jamii itapatiwa elimu sahihi kuhusu afya ya macho.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Huduma ya Macho na Daktari Bingwa wa Macho, Dkt. Yunised Claf amesema takwimu zinaonesha kuwa wanafunzi wa shule za msingi ndio wanaoathirika zaidi na changamoto za macho.
Aidha, mtaalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Lalidius Charles ameeleza kuwa lengo la wadau hao ni kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Discussion
Reader comments
0 contributions