Skip to main content

WATOTO 209 WABAINIKA KUWA NA SELIMUNDU GEITA

Watoto wachanga na wenye umri chini ya miaka mitano wapatao 209 ambao ni sawa na asilimia 4.1ya watoto 6858 waliofanyiwa vipimo vya ugonjwa wa Selimundu Mkoani Geita katika kipindi cha kati ya Mwezi Januari hadi Julai 2026 walibainika kuwa na vinasaba vya ugonjwa huo.

WATOTO 209 WABAINIKA KUWA NA SELIMUNDU GEITA
Studio Narration JAMBO FM

WATOTO 209 WABAINIKA KUWA NA SELIMUNDU GEITA

0:00 --:--

Watoto wachanga na wenye umri chini ya miaka mitano wapatao 209 ambao ni sawa na asilimia 4.1ya watoto 6858 waliofanyiwa vipimo vya ugonjwa wa Selimundu Mkoani Geita katika kipindi cha kati ya Mwezi Januari hadi Julai 2026 walibainika kuwa na vinasaba vya ugonjwa huo.

Mratibu wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza mkoa wa Geita Dkt. Glory Temba ameeleza hayo hayo Septemba 29, 2026 Mkoani Geita wakati akizungumza na wanafunzi, wazazi,walezi na watoa huduma za tiba asili katika ukumbi wa mikutano EPZA Mkoani Geita katika kilele cha maadhimisho ya mwezi wa uelewa juu ya ugonjwa wa selimundu duniani.

Dkt Glory ameeleza kwamba watoto hao ni kutoka katika halmashauri za wilaya ya Mbogwe kupitia kituo cha Afya Masumbwe,Wilaya ya Geita katika vituo vya Afya Nkome na Katoro wakati huduma za upimaji katika Manispaa ya Geita zikitolewa katika vituo vya Hospitali ya Manispaa,hospitali ya Waja na hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

‘ Kama mkoa hiyo ni aslimia kubwa sana ya kuwa na watoto wanne kati ya 100 ambao wana ugonjwa wa Sicle Cell na hii ni kwa halmashauri tatu na hatufahamu kwa halmashauri ambazo hazijafikiwa na upimaji huu wanaweza kuwa na watoto wenye changamoto hii kwa kiasi gani’ameeleza Dkt Glory

Mratibu wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza mkoa wa Geita Dkt. Glory Temba akiwasilisha mada katika kilele cha maadhimisho ya ugonjwa wa selimundu Mkoa wa Geita.

Nae Mkurugenzi wa shirika la Tanzania Sickle Cell Warriors Organization Bi. Pacskazia Thomas Mazeze,amesema Jamii inapaswa kujenga utamaduni wa Kupima ugonjwa wa selimundu (Sickle Cell) ili kuweza kubaini hali zao na kusaidia kuepuka kupata watoto wenye viashiria na vinasaba vya ugonjwa huo na kupunguza upotoshaji.

‘Huwezi kuonekana kwa macho kwamba wewe umebeba vinasaba vya ugonjwa wa Sickle Cell,kwahiyo katika uumbwaji au katika mambo ya vinasaba kwa upande wa Sickle Cell kuna watu ambao ni wazima kabisa,hawajabeba vinasaba,hawajabeba chembe chembe za ugonjwa,haowatu ni wazima kabisa tunawaita wanadamu AA,lakini kuna wale waliobeba lakini hawawezi kujua,kwahiyo bila kupima huwezi kujua kuwaumebeba chembe chembe za Sickle Cell’amesema

Mkurugenzi wa shirika la Tanzania Sickle Cell Warriors Organization Bi. Pacskazia Thomas Mazeze,akizungumza na waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya ugonjwa wa selimundu Mkoa wa Geita.

Wakizungumza baada ya kupata elimu, baadhi ya washiriki wamepongeza uwepo wa elimu hiyo na kueleza kuwa itasaidia kuendelea kujenga uelewa zaidi kwa jamii na kuachana na imani potofu juu ya ugonjwa huo.

Mwezi Septemba ni mwezi wa uelewa juu ya ugonjwa wa selimundu duniani ambapo mataifa hufanya shughuli mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kwa jamii juu ya ugonjwa huo ambapo kwa mkoa wa Geita kilele cha maadhimisho kimefanyika leo Septemba 29, 2026.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.