Skip to main content

WATENDAJI WA VIJIJI BUKOBA WAKUMBUSHWA KUFANYA MIKUTANO KILA ROBO YA MWAKA WA FEDHA

Na Clavery Christian, Bukoba - Kagera.

WATENDAJI WA VIJIJI BUKOBA WAKUMBUSHWA KUFANYA MIKUTANO KILA ROBO YA MWAKA WA FEDHA

Na Clavery Christian, Bukoba - Kagera.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima amewataka watendaji wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kuhakikisha mikutano ya vijiji inafanyika kila robo ya mwaka wa fedha, ili kuimarisha ushirikishwaji wa wananchi na kupunguza migogoro inayojitokeza katika jamii.

Sima alitoa kauli hiyo wakati wa awamu ya tano ya ziara ya kutatua kero za wananchi iliyofanyika katika kata za Izimbya, Kibirizi, Kyaitoke, Ruhunga na Rubale kuanzia Julai 15 hadi 17, 2026. 

Alisisitiza kuwa mikutano ya vijiji inapaswa kufanyika kwa mujibu wa sheria, pamoja na kuitishwa wakati wowote panapohitajika kufanya maamuzi muhimu yanayohusu maendeleo ya vijiji. Aidha, alisema maazimio yote yanayotokana na mikutano hiyo yanapaswa kutekelezwa kwa uwazi, weledi na kuwafikia wananchi wote ili kuhakikisha wanapata taarifa sahihi na hivyo kuepusha migogoro isiyo ya lazima.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Fatina Hussein Laay, aliwahakikishia wananchi kuwa wataalamu wa halmashauri wataendelea kuwahudumia kwa weledi na uadilifu ili kuharakisha maendeleo ya wananchi na halmashauri kwa ujumla.

Pia aliwataka wenyeviti wa vijiji na watendaji wote kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, sheria, kanuni na taratibu za kiutendaji katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Katika ziara hiyo, wakuu wa idara na vitengo mbalimbali walitoa elimu kwa wananchi kuhusu Bima ya Afya kwa Wote, malezi na maadili ya watoto, mbinu bora za uvunaji, utunzaji, uuzaji na usambazaji wa kahawa, mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri, pamoja na umuhimu wa kudumisha amani na mshikamano katika jamii.

Baadhi ya kero zilizopatiwa ufumbuzi katika kata hizo ni migogoro ya ardhi, uhaba wa maji katika baadhi ya vitongoji, upungufu wa walimu, ukosefu wa huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali na uchakavu wa miundombinu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.