Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi watatu, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Taarifa iliyotolewa leo, Oktoba 28, 2026 na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Shaaban Kissu imeeleza kuwa, Angeline Lubala Mabula ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, akichukua nafasi ya Beno Morris Malisa ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Rais Dkt. Samia pia amemteua Dunford George Mpelumbe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Kabla ya uteuzi huo, Mpelumbe alikuwa Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akichukua nafasi ya Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mwaimu aliyemaliza muda wake.
Katika uteuzi mwingine, Rais Samia amemteua Omar Ali Omar kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, akichukua nafasi ya Mohamed Khamis Hamad aliyemaliza muda wake.
Kabla ya uteuzi huo, Omar alikuwa Mkuu wa Idara ya Utawala, Mipango na Fedha katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume, Zanzibar.

Discussion
Reader comments
0 contributions