Skip to main content

WATATU WAFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI ARUSHA

Watu watatu wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari katika barabara ya Bypass, iliyopo Kijiji cha Kiushini wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Oktoba 30, 2026

WATATU WAFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI ARUSHA
Studio Narration JAMBO FM

WATATU WAFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI ARUSHA

0:00 --:--

Watu watatu wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari katika barabara ya Bypass, iliyopo Kijiji cha Kiushini wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Oktoba 30, 2026

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo amewataja waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Bianka Juma, Catherine Pius na Jesca Sabore ambao wote ni wanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Mringa iliyopo katika wilaya ya Arumeru.

Kamanda Masejo amesema ajali hiyo imetokea Oktoba 30, 2026 saa 11 jioni ambapo gari namba T. 415 DSN aina ya Mercedes Benz likiwa na tela namba T. 636 DSG likiendeshwa na Dereva aitwaye Abdul Seleman mkazi wa Arusha, liliacha njia na kugonga gari Na. T. 481 EKZ aina Toyota Rumion na kisha kuwagonga watembea kwa miguu watatu na kufariki dunia.

Aidha, amesema Chanzo cha ajali hiyo, ni uzembe wa dereva wa lori ambaye alikuwa anayapita magari mengine bila kuchukua tahadhari hali iiliyosababisha kwenda kugonga gari dogo lililokuwa limepaki pembeni ya barabara na kukosa uelekeo.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, limewataka madereva wote kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ikiwemo kufuata alama za barabarani, kuwa makini na watumiaji wengine wa barabara na kuchukua tahadhari zote zinazohitajika ili kuepusha ajali na vifo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.