Skip to main content

WATATU WAFARIKI KWA AJALI YA LORI KUGONGA BAJAJI, PIKIPIKI MTWARA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limemkamata na linaendelea kumhoji Ibrahimu Hamidu Joseph (32) dereva wa Lori, mkazi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, kwa kusababisha ajali iliyopelekea vifo vya watu watatu na majeruhi sita ambao walikuwa abiria wa bajaji na pikipiki.

WATATU WAFARIKI KWA AJALI YA LORI KUGONGA BAJAJI, PIKIPIKI MTWARA
Studio Narration JAMBO FM

WATATU WAFARIKI KWA AJALI YA LORI KUGONGA BAJAJI, PIKIPIKI M...

0:00 --:--

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limemkamata na linaendelea kumhoji Ibrahimu Hamidu Joseph (32) dereva wa Lori, mkazi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, kwa kusababisha ajali iliyopelekea vifo vya watu watatu na majeruhi sita ambao walikuwa abiria wa bajaji na pikipiki.

Dereva huyo alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 495 EMX aina ya Vasol likivuta tela lenye namba za usajili T 657 EPW akitokea Mtwara kuelekea Mkoa wa Lindi na anatuhumiwa kuendesha gari hilo kwa uzembe.

Tukio hilo limetokea hii leo Novemba 3, 2026 katika eneo la Magomeni Kanisani Manispaa ya Mtwara mikindani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Issa Suleiman amebainisha kuwa Chanzo cha Ajali hiyo ni uzembe wa dereva huyo wa Lori kuzipita gari zilizokuwa mbele yake bila tahadhari na kupelekea kuzigonga uso kwa uso Bajaji yenye namba za usajili MC 125 EYW na Pikipiki aina ya TVS yenye namba za usajili MC 585 CLF.

Waliofariki katika ajali hiyo Amina Salum Chinangani (42) Mkazi wa Mnolela Mkoa wa Lindi, Fatuma Yusuph Bohora (55) Mkazi wa Luhokwe Mkoa wa Lindi, Somoe Ally Hassan (40) Mkazi wa Madangwa Mkoa wa Lindi.

Majeruhi katika ajali hiyo Sharifu Mustafa Mambo (34) dereva bodaboda Mkazi wa Chipuputa Mkoa wa Mtwara, Rukia Mohamed Lipongo (34) Mkazi wa Ingwali Mkoa wa Lindi, Hajira Mfaume Mkazi wa Ingwali Mkoa wa Lindi, Esha Lipondo (37) Mkazi wa Njonjo Mkoa wa Lindi, majeruhi hawa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ligula.

Aidha majeruhi wengine Amina Ally Kilimile (39) Mkazi wa Lindi na Jamswai Dadi Nanyanga (32) dereva bajaji Mkazi wa Salemu Mtwara wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Mtwara.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linatoa wito kwa madereva na watumiaji wote wa barabara na vyombo vya moto kuendelea kutii Sheria bila shuruti na kuhakikisha wanafuata na kuheshimu alama za barabarani nakujali watuamiaji wengine wa barabara.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.