Skip to main content

WATATU WA FAMILIA MOJA, DEREVA WAHOFIWA KUFA MAJI SINGIDA

Na Saulo Stephen - Singida.

WATATU WA  FAMILIA MOJA, DEREVA WAHOFIWA KUFA MAJI SINGIDA

Na Saulo Stephen - Singida.

Aliyekuwa Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM), Mkoa wa Singida Yusuph Mwandami na watu wengine watatu akiwemo Mwenza wake, Mtoto na Dereva, wanahofiwa kufariki dunia Kufuatia gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji katika Mto Mango'nyi uliopo wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.

Ajali hiyo, imetokea usiku wa Machi 26, 2026 katika Kata ya Mang'onyi Wilayani Ikungi Mkoani Singida, wakati wakijaribu kupita katika Mto Man'gonyi uliokuwa na Maji Mengi nakupelekea gari kupoteza uelekeo hivyo kudumbukia pembezoni mwa barabara ambapo kunasadikika kulikuwa na kina kirefu.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, inasemekana mpaka muda wa Saa Kumi jioni ya leo March 27 2026 Miili ya watu wawili imepatikana huku zoezi la kutafuta miili mingine ya watu wawili ikiendelea, juhudi za kutafuta Jeshi la Polisi ili kuzungumzia tukio hilo linaendelea.

Hata hivyo, Jambo Media inaendelea kufuatilia kwa kina taarifa hizi mpaka pale zoezi la uokozi litakapokamilika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.