Skip to main content

WATATU MBARONI KWA MAUAJI YA DEREVA BODABODA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, linawashikilia watuhumiwa watatu wa mauaji ya Dereva Bodaboda, Omary Bakari (21), Mkazi wa Michese, aliyeuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mgongoni.

WATATU MBARONI KWA MAUAJI YA DEREVA BODABODA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, linawashikilia watuhumiwa watatu wa mauaji ya Dereva Bodaboda, Omary Bakari (21), Mkazi wa Michese, aliyeuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mgongoni.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma imeeleza kuwa, Watuhumiwa hao walikuwa na nia ya kutaka kunyang'anya mali ya marehemu (pikipiki), tukio hilo ambalo lilitokea Machi 21, 2026 majira ya saa 3:30 usiku katika mtaa wa Chinyoya uliopo kata ya Kilimani Jijini Dodoma.

Mara baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi lilifanya msako na kumkamata mtuhumiwa
mmoja aitwaye Sadick Jonathan (23) katika kijiji cha Mazase kilichopo Wilaya ya Chamwino Dodoma, akiwa na pikipiki ya marehemu yenye namba za usajili MC 556 FPE aina ya
Sinoray nyeusi.

Taarifa hiyo imezidi kufafanua kuwa, mara baada ya kuhojiwa mtuhumiwa alikiri kutenda kosa hilo kwa jushirikiana na wenzake wawili, Paulo Abinel (26) na Ramadhani Hamidu (35), wote wakazi wa Dodoma.

Aidha, Watuhumiwa wote wawili wamekamatwa wakiwa katika jitihada za kutoroka na kuelekea mikoa ya jirani, na watafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.