Skip to main content

WATANZANIA WAHIMIZWA KUFANYA MAZOEZI KUIMARISHA AFYA

Na Gideon Gregory - Dodoma.

WATANZANIA WAHIMIZWA KUFANYA MAZOEZI KUIMARISHA AFYA

Na Gideon Gregory  - Dodoma.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amewataka wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu wa nchi, akisisitiza kuwa ndiyo nguzo kuu ya kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Abdulla ameyasema hayo leo Aprili 18, 2026 Jijini Dodoma wakati akizungumza na washiriki wa Bunge Marathon iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri.

“Niendelee kuwasisitiza wananchi kulinda na kutunza amani ya nchi kwani ndiyo nguzo kuu ya maendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kutamalaki,” amesema.

Pia, amesisitiza Watanzania kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya na kuongeza uwezo wa kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Ameongeza kuwa: “Amani ndiyo msingi imara wa Taifa; tusipoilinda, ikipotea ni kazi sana kuirejesha. Hivyo, tusiache ikapotea kwa maslahi mapana ya Taifa.”

Kuhusu mazoezi, Abdulla amesema ni muhimu kwa kuwa husaidia kujenga afya bora na kuongeza uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji zinazochangia ukuaji wa uchumi.

Amewapongeza wabunge na wananchi waliojitokeza kushiriki marathon hiyo, huku akisifu Bunge la Tanzania kwa kuandaa tukio hilo kwa ufanisi mkubwa.

“Maandalizi yaliyofanyika katika tukio hili ni ya kiwango cha kimataifa. Niwapongeze sana wabunge na wananchi mliojitokeza kushiriki. Nasisitiza wananchi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya na kuongeza nguvu katika shughuli za uzalishaji,” amesema.

Kwa upande wake Spika wa Bunge, Mussa Zungu, amesema mazoezi ni muhimu kwa kuwa yanakutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali na hivyo kuimarisha umoja na mshikamano.

Amesisitiza wananchi kuendelea kudumisha umoja na mshikamano ili kuhakikisha nchi inapiga hatua za maendeleo.

Awali, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, amesema michezo husaidia kuimarisha mahusiano kati ya watumishi wa serikali na wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.