Skip to main content

WATANZANIA TUUNGANE KUOKOA MAISHA YA WAGONJWA WENYE UHITAJI - DKT. MWIGULU

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania, taasisi za umma na binafsi, mashirika na wadau wa maendeleo waungane na Serikali katika kuwezesha matibabu ya upandikizaji wa figo na uloto kwa wananchi wasiokuwa na uwezo, ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma hizo za kibingwa.

WATANZANIA TUUNGANE KUOKOA MAISHA YA WAGONJWA WENYE UHITAJI   - DKT. MWIGULU

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania, taasisi za umma na binafsi, mashirika na wadau wa maendeleo waungane na Serikali katika kuwezesha matibabu ya upandikizaji wa figo na uloto kwa wananchi wasiokuwa na uwezo, ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma hizo za kibingwa.

“Hiki ni kitendo cha kiungwana, cha ibada na kinachogusa maisha ya Watanzania. Nawapongeza Umoja wa Wanawake Tanzania kwa kuitikia wito huu na kuwa sehemu ya kuokoa maisha ya wananchi,” amesema.

“Tunachokifanya leo ni kurejesha matumaini kwa wagonjwa na familia zao. Kila anayeguswa na jambo hili aendelee kushiriki ili wananchi wengi zaidi wanufaike na huduma hizi muhimu,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo jana (Alhamisi, Julai 16, 2026) katika hafla ya Okoa Maisha Gala iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kushirikiana na Hospitali ya Benjamin Mkapa katika Ukumbi wa Mabele Hall, Jenerali Venance Mabeyo Complex, jijini Dodoma.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwekeza katika sekta ya afya kwa kuboresha miundombinu, kuongeza vifaa tiba na kuimarisha huduma za kibingwa ili Watanzania wengi zaidi wapate matibabu ya kiwango cha juu ndani ya nchi.

Awali, Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, alisema Serikali itaendelea kuboresha huduma za kibingwa nchini kwa kuimarisha miundombinu ya afya, vifaa tiba na rasilimali watu, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono Mfuko wa Matibabu ya Upandikizaji wa Figo na Uloto.

Katika hafla hiyo, jumla ya shilingi bilioni 2.225 zilipatikana kupitia michango na ahadi za wadau mbalimbali kwa ajili ya kuunga mkono Mfuko wa Matibabu ya Upandikizaji wa Figo na Uloto. Fedha hizo zitatumika kusaidia matibabu ya wagonjwa pamoja na kuboresha miundombinu ya huduma za upandikizaji wa figo na uloto.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.