Na Cecilia Shiratu, Kyerwa - Bukoba .
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mlezi wa mkoa wa Kagera, Ashatu Kijaji ameahidi kuwa ifikapo 2030 wananchi wote nchini Tanzania watakuwa na nishati Bora ya umeme kwa kuhakikisha kuwa Vitongoji vyote ambayo havikufikiwa na huduma ya umeme vinafikiwa.
Kijaji ameongeza kuwakitongoji Cha Nyakanga kata ya Rusumo wilayani Ngara kipo kwenye mpango wa mradi endelevu wa kupata umeme, hivyo ndani ya mwaka huu tunatarajia kupata takwimu juu ya upimaji na kufanya tathimini Ili kitongoji hicho kipate nishati safi kwa maendeleo ya kiuchumi ya jamiii na taifa kwa ujumla.

Msimamizi wa miradi na wakala wa nishati vijijini mkoa wa Kagera muhandisi Oscar Migani ameleza kuwa kitongoji Cha Nyakanga kipo katika mradi unaondelea, ili kuhakikisha umeme unafika kwenye kitongoji hicho mapema.
Aidha, amekitembelea na kufanya tathimini ya kiwango Cha umbali kutoka Kata ya Rusumo ambopo umeme ulipoishia mpaka kitongoji Cha Nyakanga, Ili kuhakika kitongoji hicho kinapata umeme haraka iwezekamavyo hata hivyo watahakikisha Vitongoji vyote visivyokua na umeme vinapata umeme kwa awamu.

Jakobo Zakayo na Fedelesa Emanuel ni wananchi wa kitongoji Cha Nyakanga kata ya Rusumo wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu barabara, maji na umeme ambazo zinawafanya wananchi kutumia gharama kubwa katika sekta ya usafirishaji na kupeleka mlipuko wa magonjwa mbalimbali hivyo wameiomba serikali kuwapatia Maji safi na salama pia nishati safi Ili kukuza uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla.

Discussion
Reader comments
0 contributions