Skip to main content

WASTANI WA PATO LA TAIFA KWA MTU NI MILIONI 3.5 - PROF. MKUMBO

Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema wastani wa Pato la Taifa kwa Mtu umeongezeka kwa asilimia 7.4 na kufikia shilingi 3,544,124 (dola 1,390) mwaka 2025, ikilinganishwa na shilingi 3,299,637 (dola 1,264) mwaka 2024.

Prof. Mkumbo ameyasema hayo wakati akiwasilisha Bungeni taarifa ya hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2025 pamoja na mpango wa maendeleo wa 2026/2027, hii leo Juni 11, 2026.

Amesema, “kutokana na mwenendo huo, wastani wa Pato la Taifa kwa Mtu uliongezeka kwa asilimia 7.4 na kufikia shilingi 3,544,124 (dola 1,390) mwaka 2025 ikilinganishwa na shilingi 3,299,637 (dola 1,264) mwaka 2024,”amesema Prof. Kitila.

Aidha, ameongeza kuwa, maboresho ya takwimu za Pato la Taifa yamefanyika kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ambapo mwaka wa kizio umebadilishwa kutoka 2015 hadi 2019 ili kuakisi hali halisi ya uchumi wa sasa.

“Kwa mujibu wa takwimu mpya, Pato halisi la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 5.9 mwaka 2025 kutoka asilimia 5.6 mwaka 2024 huku kwa bei za mwaka 2019, Pato la Taifa likifikia shilingi trilioni 234.104 (dola bilioni 91.81) mwaka 2025, ikilinganishwa na trilioni 211.975 (dola bilioni 81.2) mwaka 2024,” aliongeza Mkumbo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.