Skip to main content

WASIOREJESHA MIKOPO MUSOMA WAPEWA SIKU 21

Na Adam Msafiri - Mara.

WASIOREJESHA MIKOPO MUSOMA WAPEWA SIKU 21

Na Adam Msafiri - Mara.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka, ametoa siku 21 kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu vinavyodaiwa kushindwa kurejesha mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 371, kuhakikisha vinakamilisha marejesho kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa.

Fedha hizo zinadaiwa kuwa sehemu ya mikopo iliyotolewa katika mwaka wa fedha 2024/2025 kupitia mpango wa uwezeshaji wa makundi maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.

Chikoka ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya kukabidhi mikopo mipya yenye thamani ya shilingi milioni 298.5 kwa vikundi 21 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Amesema urejeshaji wa mikopo kwa wakati ni muhimu ili kuwezesha makundi mengine kunufaika na mpango huo wa serikali.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango huo, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Frank Mwegoha, amesema baadhi ya vikundi vinaendelea kurejesha mikopo kwa wakati, huku vingine vikichangia kuongezeka kwa madeni kutokana na kutotekeleza wajibu wao wa marejesho.

Kwa upande wao, baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo wameahidi kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha wanarejesha fedha hizo kwa wakati ili kutoa nafasi kwa wengine kunufaika na fursa hiyo.

Takwimu za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma zinaonyesha kuwa zaidi ya shilingi milioni 900 zimetolewa kama mikopo kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.