Skip to main content

WASIOFANYA USAFI WA MAZINGIRA SHINYANGA KUCHUKULIWA HATUA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita leo tarehe 25 September 2026 amewaongoza wananchi kufanya usafi katika soko la wajasiliamali la Ibinzamata lililopo katika Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni uzinduzi wa kampeni ya usafi wa mazingira kila siku ya jumamosi,lakini pia kuendelea kuchukua tahadhari juu ya mvua za El- nino zinazotarajiwa kuanza Oktoba 2026.

WASIOFANYA USAFI WA MAZINGIRA SHINYANGA KUCHUKULIWA HATUA
Studio Narration JAMBO FM

WASIOFANYA USAFI WA MAZINGIRA SHINYANGA KUCHUKULIWA HATUA

0:00 --:--

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita leo tarehe 25 September 2026 amewaongoza wananchi kufanya usafi katika soko la wajasiliamali la Ibinzamata lililopo katika Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni uzinduzi wa kampeni ya usafi wa mazingira kila siku ya jumamosi,lakini pia kuendelea kuchukua tahadhari juu ya mvua za El- nino zinazotarajiwa kuanza Oktoba 2026.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la usafi RC Mhita amesema Serikali Mkoani Shinyanga imedhamiria kuanza kuchukua hatua kali za kisheria ikiwemo faini kwa kaya zitakoshindwa kutekeleza zoezi la usafi katika maeneo yao.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita

Amesema wenyeviti wote wa vitongoji,vijiji na mitaa waweke taratibu za usafi katika maeneo yao na kuzisimamia na kwamba kila jumamosi wahakikishe maeneo yao yanafanyiwa usafi na kuanisha kwamba kwa sasa katika Mkoa wa Shinyanga kutakuwa kukifanyika tathimini ya kubaini vitongoji,vijiji na mitaa inayoongoza kwa usafi na kwale watakao kuwa wakifanya vibaya hatua stahiki zitachukuliwa.

Amesisitiza kuwa mbali na mkakati wa kutoa elimu kwa umma bado viongozi ikiwemo wenyeviti wa vijiji na mitaa wanalo jukumu la kuwatoza faini wote watakao bainika kukwamisha azma ya Serikali ya usafi wa mazingira.

Mkuu wa Wilaya Shinyanga, Wakili Msomi Julius Mtatiro

Akipokea maelekezo hayo mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro ameelezea utayari wa viongozi na wananchi wilayani humo katika suala zima la utunzaji wa mazingira na usafi ili kuendeleza hadhi ya manispaa ya Shinyanga kuwa kinara kwa miaka mitatu mfululizo kitaifa katika suala zima la usafi na utunzaji wa mazingira.

Sehemu ya Wananchi waliojitokeza kushiriki katika zoezi la usafi.

Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya usafi katika eneo hilo akiweno Tatu almasi mkazi wa manispaa ya Shinyanga amesema wamepokea maagizo ya mkuu wa mkoa na kwenda kuyatekeleza ili kuondoka na athari za mvua za elnino.

Mkazi wa Manispaa ya Shinyanga, Tatu Almas.

Kwa upande wake Husna Ally mkazi wa Ndala katika manispaa hiyo amehaidi kwenda kuhamasisha jamii katika maeneo yake ili waweze kufanya usafi katika mitaro na maeneo yote yaliyoziba kutokana na uchafu ili kuepusha vifo pamoja na madhara mengine .

Mkazi wa Ndala Shinyanga, Husna Ally

Aliyehudhuria zoezi hilo la usafi ni Habiba Jumanne, ambaye amewaomba wananchi wote wanaoishi katika maeneo ya mabondeni wahame kwa muda kuepeka madhara yatokanayo na mvua hizo na kwamba wawe tayari kutoa taarifa katika mamlaka husika waoanapo madhara pindi msimu wa mvua utakapoanza.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.