Serukali Nchini, imepiga marufuku Watu wasio na taaluma ya mipangomiji kufanya shughuli zinazohusiana na taaluma hiyo, kwani kazi hizo zinapaswa kufanywa na wataalam wenye sifa stahiki kisheria na taratibu.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kasper Mmuya wakati wa Mkutano Mkuu wa 11 wa Wataalam wa Mipangomiji jijini Arusha.
Amesema, ushiriki wa wataalam wenye sifa na weledi ni muhimu katika kuhakikisha miji inakua kwa utaratibu, kwa kuzingatia sheria.

Mmuya ameongeza kuwa, hatua hiyo itasaidia kuimarisha usimamizi wa maendeleo ya miji na kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na mipango isiyozingatia taratibu za kitaaluma.
Awali, Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB), Martha Mkupasi alisema, Bodi inaendelea kusimamia na kudhibiti taaluma ya mipangomiji nchini.
Mkutano huo, umewakutanisha wadau hao kujadili masuala yanayohusu maendeleo ya taaluma hiyo, kubadilishana uzoefu na kuangazia matumizi ya teknolojia za kidijitali ili kuimarisha udhibiti wa ukuaji wa miji.
Discussion
Reader comments
0 contributions