Skip to main content

WASICHANA ZAIDI YA 250 WALIOKATISHA MASOMO GEITA WATENGENEZEWA TABASAMU

Na Ibrahim Rojala - Geita.

WASICHANA ZAIDI YA 250 WALIOKATISHA MASOMO GEITA WATENGENEZEWA  TABASAMU

Na Ibrahim Rojala - Geita.

Zaidi ya Wasichana 250 kutoka kata tano Mkoani Geita, waliokatisha masomo kutokana na ujauzito, wanatarajiwa kunufaika na Mradi wa Justice for Survivors, unaolenga kuwawezesha kiuchumi na kijamii pamoja na kuwasaidia kupata haki baada ya kupitia ukatili wa kijinsia.

Akizungumza Katika Ukumbi wa Mikutano wa Masuka, Halmashauri ya Manisapaa ya Geita wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Human Dignity Initiative (HDI), Wakili Walta Carlos, amesema mradi utatekelezwa katika kata za Nyawilimilwa, Lwamgasa, Nkome (Wilaya ya Geita) pamoja na Mtakuja na Nyankumbu (Manispaa ya Geita) akieleza kuwa utekelezaji wake utahusisha viongozi kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa, ili kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

“Katika kila kata tutakuwa na vikundi vya mabinti ambao wamekatisha masomo kwasababu za utauzito kuanzia 10 mpaka 15 na mabinti hao pia watakuwa wanapata elimu ya kujikinga zaidi na ukatili wa kijinsia kwasababu tayari wao ni manusura kwahiyo kupitia programmu hizo tutafanya kitu kinaitwa uwezeshaji wa kiuchumi na kijamii kupitia vikundi”amesema Wakili Walta

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Geita, Frank Mushi, amesema mradi huo utatoa msaada wa kisheria kwa manusura, kuwasaidia kukabiliana na vitisho kutoka kwa watuhumiwa wa ukatili na kuwezesha hatua za kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria.

“Ukiangalia programmu hii ambayo wanakwenda kuianzisha itasaidia katika mambo mbalimbali mojawapo ni kutoa msaada wa kisheria, lakini vile vile kutoa elimu kwenye jamii kwasababu tunafahamu kama kuna changamoto ya waliofanyiwa ukatili kuficha taarifa, kuogopa kutoa taarifa na hiyo inasababishwa na vitisho ambavyo wanavipata aidha kutoka kwa waliotenda ukatili au kwa wazazi baada ya  kukubaliana mambo fulani na aliyetenda ukatili,” amesema Frank.

 Kwa upande wake, Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Manispaa ya Geita, Joyce Mataba, amesema utoaji wa mitaji kwa wasichana hao utawajengea uwezo wa kujitegemea na kuwahamasisha wahanga wengine kuvunja ukimya badala ya kuficha vitendo vya ukatili vinavyowakabili.

“Kata ya Mtakuja ina shughuli za uchimbaji na pia kwa sehemu kiasi pia kata ya Nyankumbu vivyo hivyo kwa mradi ambao wameamua kuufanya katika kata zetu ni maeneo sahihi kabisa na walengwa watapatikana katika eneo lile,na pia ninashukuru Shirika la HDI kwa kuona mabinti wa kata ya Nyankumbu, imekuwa ni kata yenye shughuli mbalimbali za kijamii na yamkini changamoto ya hawa wahanga wa ukatili ikawepo kwenye kata zetu, kwahiyo mimi ninaamini kabisa kwa kata ya Nyankumbu na Kata ya Mtakuja ni sehemu sahihi ya kutekeleza shughuli zao,” amebainisha Joyce.

 Naye Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Geita, Michael Agustino, amesema mradi huo pia utasaidia kuboresha malezi ya watoto wa wasichana hasa waliotelekezwa na wazazi wenza, hali ambayo imekuwa changamoto kubwa katika jamii.

“Kumekuwa na wahamiaji wengi ambao wanatoka katika maeneo mengine kwaajili ya kutafuta fursa mbalimbali kama mnavyojua eneo letu la Geita lina fursa ya madini lakini pia kuna shughuli mbalimbali za kibiashara kwasababu pia tuko jirani na mgodi mkubwa wa GGML,shughuli za kiuchumi ni nyingi sana kwahiyo kuna wadada wanaokuja kutoka katika maeneo mbalimbali ambao kwa kiasi kikubwa wababa wamewatelekeza na watoto wadogo ambao wanakuja kuanza nao maisha,” amebainisha Michael.

Mradi wa Justice for Survivors ni wa matazamio ukitarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja ndani ya kata tano zilizochaguliwa  na   ili kuleta ufanisi katika utekelezwaji wake umetambulishwa kwa watendaji kuanzia ngazi kata, ili kuwajengea uwezo wa namna ya utekelezwaji wake ukitarajiwa kuongea uelewa wa kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia,kuibua vinara wa kupinga ukatili wa kijinsia, kuongeza ubunifu na uelewa wa masuala ya ujasiriamali kwa zaidi ya wasichana 250.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.